RUANGWA-LINDI
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ametembelea na Kukagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa vijiji 34 vya wilaya ya Ruangwa na Vijiji 21 vya Wilaya ya Nachingwea kutoka Chanzo cha mto Nyangao.
Aidha, Akiwa eneo la Mradi Aweso amemtaka mkandarasi STC Construction kuanza mara moja kazi ya ujenzi kwenye chanzo ambako ndio moyo wa Mradi akielekeza kwa kumpigia simu mkandarasi aripoti Kwa Mkuu wa Mkoa wiki hii na kuingia site kuanza kazi.
Katika hatua nyingine Aweso ameeleza kwamba Mradi ulianza tarehe 18/02/2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 28/04/2025 ambapo unatarajiwa kuwanufaisha wananchi 128,657 wa Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea na Hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu Shilingi 119,153,611,787
Katika hatua nyingine Aweso Akizungumza baada ya ukaguzi wa Mradi huo ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi hususani ujenzi wa Tenki kubwa na kueleza kwamba kazi nzuri inaendelea kufanyika.