Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amepokelewa Mkoani Shinyanga kwa staili ya aina yake na ya kipekee.
Makonda amepokelewa kwenye Bulldozer huku akiwa amevalia mavazi ya uchimbaji madini.
Kupokelewa kwa Bulldozer na mavazi hayo ya uchimba madini inadhihirisha wazi Madini ya Chama Cha Mapinduzi kwa maana ya sera zenye kuijenga Tanzania imara zimewasili mkoani Shinyanga na Bulldozer likimaanisha ukarabati katika maeneo yote ya Serikali ambayo utendaji kazi unasuasua katika kumsadia kazi Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kubaini na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazokwamisha miradi na maendeleo ya taifa.