Polisi Kata wa Kata ya Nambizo Wilayani Mbozi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Issa Mudu akizungumza na mtoto wa Shule ya Msingi Utambalila baada ya kuwapa elimu ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto leo Januari 26, 2024.
Mkaguzi Mudu aliwaambia wanafunzi hao wasikae kimya wala kusita kutoa taarifa kwa jambo lolote ambalo watalitilia mashaka au la ukatili dhidi yao.