Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Shule ya Msingi Dodoma English Medium leo Januari 25, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipanda mti wakati akizindua zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Shule ya Msingi Dodoma English Medium leo Januari 25, 2024.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akipanda mti katika Shule ya Msingi Dodoma English Medium wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Januari 25, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi la upandaji wa miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Shule ya Msingi Dodoma English Medium leo Januari 25, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwanawisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Dodoma English Medium wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji wa miti kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika eneo la shule hiyo leo Januari 25, 2024.
……………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amehimiza usafi wa mazingira katika maeneo yanayoizunguka jamii ili kujikinga na maradhi ya hususan kipindupindu.
Amezielekeza mamlaka za Serikali za Mitaa kuwasimamia wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la usafi katika mitaa yote ili kuifanya kuwa safi.
Dkt. Jafo ametoa maelekezo hayo wakati akizindua zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika katika Shule ya Msingi ya Dodoma English Medium leo Januari 25, 2024, lililoambatana na upandaji wa miti 60 katika eneo la shule.
Akizungumza na viongozi, wanafunzi na wananchi, amesema amesema suala la upandaji miti katika maeneo yanayoizunguka jamii ni jukumu la kila mwananchi katika kulinda uhai.
“Kwa kutambua Muungano wetu ni tunu ya Taifa letu, na msingi wa maisha ya Watanzania, tumechukua hatua za kuulinda na kuuenzi ikiwa ni pamoja na kuendelea kuelimisha umma kuhusu umuhimu wake katika historia ya Taifa letu.
“Ofisi ya Makamu wa Rais imeona ni vema maadhimisho haya yaende sambamba na shughuli za hifadhi ya mazingira hususani upandaji miti kote nchini. Kila taasisi na wananchi wote katika maeneo yetu wanatakiwa kupanda miti ya kumbukumbu ya miaka 60 ya Muungano,” amesema.
Dkt. Jafo ameongeza kuwa upandaji wa miti kuelekea maadhimisho ya Muungano unafanyika kuendeleza kampeni ya Serikali ya hifadhi ya mazingira hususani, kupanda na kutunza miti na kusema kuwa kama tulivyoungana kulinda uhuru, utamaduni na utaifa wetu, tunahimizwa tuungane kulinda mazinigra yetu.
Aidha, amesisitiza kuwa kila mwananchi anatakiwa kupanda mti wa kumbukumbu ya Muungano na kila taasisi katika ngazi zote, kitaifa, kimkoa na mamlaka za Serikali za Mitaa, inatakiwa kupanda miti isiyopungua 60 kama alama ya miaka 60.
Kwa upande wa Jiji la Dodoma shughuli hiyo ya upandaji miti ni muendelezo wa Kampeni ya Kukijanisha Jiji la Dodoma ili Kuongeza uoto wa asili katika Makao Makuu ya Nchi.
Zoezi la upandaji wa miti limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wakiwemo Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Mkuu wa Wilaya hiyo Jabir Shekimweri, Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Prof. Davis Mwamfupe na watumishi na wananchi ambapo litaendelea katika maeneo tofauti hadi Januari 30, 2024 huku lengo likiwa ni kupanda miti 250.
Katika eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Megereza, Msalato ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni ataongoza makamanda na askari wa jeshi hilo.
Katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda ataongoza zoezi hilo, Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ataongoza.
Halikadhalika, katika Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Eneo la Chamwino Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Stagomena Tax ataongoza na mwisho itakuwa Januari 30 katika Viunga vya Mji wa Serikali Eneo la Mtumba ambapo wakuu wa taasisi zenye ofisi wataongoza watumishi na wadau wa mazingira kupanda miti.