Waandishi wa habari wa Dar es Salaam wamepewa semina juu ya utambuzi wa magonjwa ya kichocho cha tumbo na kichocho cha kibofu cha mkojo ili waweze kuielimisha jamii kupitia kalamu zao kutokana na magonjwa hayo kuwa miongoni mwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Semina hiyo imefanyika leo Jumatano Januari 24, 2024 katika ukumbi wa Chama Cha Wanasheria Tanzania (TLS) Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye semina hiyo Afisa Programu Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele amesema kichocho cha kibofu cha mkojo kinaambukizwa na minyoo inayopatikana kwenye maji yaliyotuama kama vile mabwawa, madimbwi au ziwa na wanaingia kwenye mwili wa binadamu kupitia ngozi.
Amesema binadamu ndio chanzo cha kwanza kabisa kusambaza ugonjwa huo kwani yeye ndio mbebaji wa minyoo na anaeneza kwa njia ya kujisaidia katika vyanzo vya maji.
Ameeleza Pamoja na kutoa kinga tiba kwa wananchi lakini wanapambana pia na usafi wa mazingira ili kuweka mazingira ya ugonjwa huo kutojirudia.
“Binadamu huambukizwa ugonjwa huo kwa kugusa maji hayo,kuogelea au shughuli za umwagiliaji wa mazao pamoja na kufua,kinga tiba hupunguza maambukizi endapo mazingira yataboreshwa na kuwa masafi ndio maana huwa tunawahimiza wananchi wawe na vyoo bora na wavitumie kwakuzingatia usafi”, amesema Njau
Amesema magonjwa ya kichocho nitofauti na magonjwa mengine kama maralia kutokana na dalili zake kuchukua muda kuonekana,dalili kubwa za ugonjwa huu ni kupata homa,maumivu ya tumbo na unapojisaidia haja kubwa inakuwa imechanganyikana na damu.
“Tunawashauri wagonjwa wanapoona hizi dalili wawahi kwenye vituo vya afya kwaajili ya uchunguzi, ushauri na matibabu”, amesema Njau.
Akizungumza kichocho chatumbo Isaac Njau amesema magonjwa anakuwa na maumivu sehemu ya chini ya tumbo au chini ya kitovu na hivyo kupelekea kukojoa damu
Ugonjwa wa kichocho unaweza usioneshe dalili yoyote katika hatua za awali lakini mwili utaendelea kuhathirika hivyo tunashauri kumeza Kinga tiba za ugonjwa huo pale zinapotolewa kwenye jamii.
” Huwa tunatoa Kinga tiba kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kutokana na michezo yao mbalimbali wanayokuwa nayo hivyo kupelekea kuwa na maambukizi kuliko watu wazima tunapowapa Kinga tiba tunakuwa tumeisaidia jamii kwa kiasi kikubwa”,
Madhara ya kichocho kwenye mfumo wa chakula ni kuharibiwa kwa utumbo mkubwa, kupata saratani ya tumbo ambapo ini linaharibika,tumbo linajaa maji pamoja na kutapika damu.
“Kwenye mfumo wa mkojo Figo inajaaa maji kunakuwa na uvimbe kwenye figo pia unaweza kupata saratani ya kibofu cha mkojo