Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Januari, 2024.
Pamoja na Mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kimahusiano ya kihistoria katika nyanja mbalimbali ikiwemo Kidiplomasia, elimu, sekta ya afya, utalii pamoja na Jeshi.
Kuhusu mahusiano ya Kibunge, Viongozi hao wamezungumzia namna bora ya kufanya mashirikiano ya kubadilishana uzoefu wa teknolojia ya mawasiliano huku wakiangazia ukuaji wa akili bandia unaoonekana kujitokeza duniani kote.