Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ambaye ni Chifu wa Wamasai amepokelewa kw kishindo na wakazi wa Makuyunk alipofika Wilayani Monduli akiwa njiani kuelekea Mkoani Manyara.
Kwa heshima kubwa ya kuwa Chifu wa Wamasai aliyopewa jana akiwa Usa River – Arumeru , Mwenezi Makonda ameuthibitishia umma kuwa yeye ni Laigwanani wa kweli kwa kushiriki kucheza ngoma ya kabila hilo mbele ya Wanaume na Wanawake wa Kimasai.