Timu ya Taifa ya Cameroon imefanikiwa kumaliza nafasi ya pili katika Kundi C katika Fainali za Mataifa ya Afrika 2023 baada ya kushinda mabao 3- 2 dhidi ya timu ya Taifa Gambia katika mchezo wa mwisho ya kundi hilo uliopigwa Januari 23, 2024 nchini Ivory Coast.
Toko-Ekambi bin aliifungia Cameroon, huku Gomez pia akijifunga kabla ya Wooh kufunga bao la ushindi kwa muda wa nyongeza kwa timu hiyo inayofundishwa na Rigobert Song.
Kwa upande wa timu ya Taifa ya Gambia mchezaji Jallow Ablie na Colley Ebrima walifanikiwa kuifungia timu yao katika mchezo huo.
Kwa matokeo haya Cameroon watakuwa na kibarua Cha kuwakabidhi Nigeria katika mchezo wa hatua ya 16 bora utakaochezwa Januari 27, 2024.
Mchezo mwengine wa kundi C timu ya Taifa ya Senegal imefanikiwa kuichapa timu ya Taifa ya Guinea mabao 2-0 na kuwafanya kutinga hatua ya 16 bora wakiwa kinara katika kundi hilo baada ya kushinda michezo yote mitatu na kukusanya pointi 9.
Katika kundi D timu ya Taifa ya Angola ilifanikiwa kushinda mabao 2- 0 dhidi ya timu ya Taifa ya Burkina Faso, huku timu ya Taifa ya Mauritania ikifanikiwa kupata matokeo ya goli moja dhidi ya Algeria.
Kufatia matokeo hayo timu ya Taifa ya Angola na Burkina Faso zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 Bora kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2023.