Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye amewasili nchini kwa ziara ya Siku Tatu.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya ziara ya kikazi ya Siku Tatu. Katika uwanja huo amepokewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akitambulisha viongozi mbalimbali waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpokea Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye amewasili nchini kwa ziara ya siku Tatu.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakisalimia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Balozi Chen Mingjian katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kabla ya kuwasili kwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong.
……………………..
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo ameongoza mapokezi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku Tatu.
Akiwa nchini, Mhe. Guozhong anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Pia, atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na eneo la makaburi ya Wataalam wa kichina waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA pamoja na Makumbusho ya Taifa.