VICTOR MASANGU,MKATA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Kiula kingu amefika katika kata ya Mkata iliyopo halmashauri ya Tanga Vijijini kutekeleza kwa vitendo agizo lililotolewa na Waziri wa Maji Juma Aweso la kutaka kuimaliza kero na changamoto ya maji ambayo inawakumba wakazi wa eneo hilo.
Aweso alitoa agizo hilo
wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Paul Makonda ambapo msafara wake uliposimama katika eneo hilo la Msata ukitokea Mkoani Pwani na kuagiza huduma ya maji safi na salama iwafikie wananchi hao.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika eneo hilo ikiwa ni katika kutekeleza maagizo hayo ya Waziri Kaimu mtendaji huyo wa Dawasa Kiula alisema kwamba kwa sasa wakazi wa eneo hilo la Msata wanapata maji ambayo sio toshelevu kutoka na kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi ya wananchi.
“Kimsingi tumefika katika eneo hili la Msata mashariki na hii ni hii tunatekeleza wito na maagizo ambayo yametolewa na Waziri wa maji Juma aweso kwa hivyo tumefika ili kuitatua changamoto hii ya maji,”alisema Kingu.
Kingu alibainisha kwamba katika eneo hilo sio kwamba halina huduma ya maji safi na salama isipokuwa maji yaliyipo kwa sasa hayawezi kutosheleza kutoka na kuwa na ongezeko kubwa la wakazi ambao wanafikia zaodi ya elfu 90.
Aidha aliongeza kuwa mipango ambayo inafanyika kwa sasa na Dawasa ni kufanya jitihada za haraka katika kupeleka huduma ya maji kupitia chanzo cha maji kilichopo kutoka tenki la maji lililopo kijiji cha Manga.
Pia alibainisha kuwa sambamba na kuongeza wingi wa maji pia Mamlaka itahakikidha itaboresha miundombinu yote ya maji ambayo ipo katika kata ya Mkata ili iweze kuhudumia wananchi kwa urahisi.
“Ukiangalia eneo hili la mkata wakazi wanazidi kuongezeka zaidi ukilinganisha na siku za nyuma hivyo ni lazima tuweke mipango ya kuboresha miundombinu ya maji na kuvuta maji kutoka maeneo ya jirani na hii itasaidia sana kwa wananchi kupata maji ya uhakika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Mkata Mashariki , Zamini Kafuluma ameupongeza uongozi wa DAWASA kwa kufika katika eneo hilo kwa lengo la kujionea na kutekeleza maagizo ambayo yametolewa na Waziri wa Maji pamoja na Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa.
Mwenyekiti huyo aliongeza kitendo walichokifanya Dawasa ni kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo kwa lengo la kuhakikisha wanasogeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
Siku chache zilizopita Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi ,(CCM) Taifa Paul Makonda alipokuwa katika ziara yake ya kikazi akiwa na Waziri wa Maji Juma Aweso walitoa maagizo kwa uongozi wa Dawasa kufika katika eneo la Msata mashariki ili kutatua ya maji kwa wananchi jambo ambalo limeanza kutekelezwa kwa vitendo na Dawasa.