Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amebainisha kuwa yeye ndiye alimshawishi Ndugu. Albert Msando Mkuu wa wilaya ya Handeni ili kutoka ACT na kuhamia Chama Cha Mapinduzi kwakuwa aliona kujituma kwake na hamu ya kutaka kuona maendeleo yanasonga mbele katika Taifa letu.
Mwenezi Makonda amebainisha hilo leo tarehe 20 Januari, 2024 alipokuwa akizungumza na maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Handeni baada ya kupokelewa kwa shangwe kwa ziara ya siku 2 mkoani Tanga ambapo alisikiliza changamoto zao ambazo alimtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Albert Msando kuzitolewa majibu ambapo naye alifanya hivyo na kupelekea Wananchi kuridhishwa na maelezo yake.
Akizungumza na Wananchi hao wa Handeni, Mwenezi Makonda ametoa wito wa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti bingwa Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari. Samia Suluhu Hassan.