Timu ya Taifa ya Cape Verde imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora katika mashindano ya Mataifa ya Afrika AFCOn 2023 baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa raundi ya pili uliopigwa leo Januari 19,2024 nchini Ivory Coast.
Mchezo huo ilijaa mabao ya kuvutia, kuanzia bao la Bebe katika dakika ya 32. Kwa mkwaju mkali wa faulo na kmshinda mlinda mlango Ernan Siluane, ambaye hakuweza kuumudu shuti hilo.
Kipindi cha pili, ulinzi mbovu kutoka timu ya Taifa ya Msumbiji ulimruhusu Ryan Mendes kufunga bao la pili la Cape Verde katika dakika ya 51.
Hatimaye, Kevin Pina aliifungia timu yake bao lingine la kuvutia, akifumua shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari katika dakika ya 69 na kupata ushindi mnono.
Cape Verde kwa sasa inaongoza Kundi B, ikizipita timu kama Misri na Ghana, hivyo kujihakikishia nafasi ya kuingia hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Pia timu ya Taifa ya Senegali nayo imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON baada ya kuichapa Cameroon mabao matatu kwa moja.