Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa kamati ya hamasa ya timu za Taifa,kikao hicho kimefanyika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Januari 17, 2024. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameipongeza kamati hiyo kwa kufanikisha harambee ya kuzichangia timu za Taifa iliyofanyika Januari 10, 2024 kwenye ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)