Na Sophia Kingimali
Umoja usio rasmi wa vyama 13 vya siasa visivyo na uwakilishi bungeni wamewataka viongozi wa clChama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kusitisha maandamano yao waliyopanga kuyafanya januari 24 nchi nzima badala yake warudi mezani na kujadiliana ili kuepusha uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo januari 17,2024 jijini Dar es salaam mwenyekiti wa umoja huo ambae pia ni katibu mkuu wa chama cha DP Abdul Mluya amesema kuwa hatua walioichukua CHADEMA yakuitisha maandamano ni hatua mbaya na inakusudi la kuvunja Amani ya nchi ambayo ni tunu kwa Taifa.
“Malengo yetu kama vyama ni kuanzisha malengo mahususi dhidi ya amani na umoja wa kitaifa njia hii ya maandamano inakidhana na utamaduni wetu kwani inaviashiria vya uvunjifu wa amani ni haki sawa kuandamana lakini sio kila haki uitumie nyingine zinamadhara kwa taifa”amesema Mluya.
Aidha Mluya ametoa rai kwa viongozi wa dini kusimama katika njia zao badala yake wasitumie dini kuendesha siasa kwa kwa taasisi ya Dini ni kubwa na inaheshimika”
“Tuwatake viongozi wa dini wasimame sehemu moja ili hata wakitoa hoja tujua tunajibu hoja kama siasa au dini lakini si kuchanganya na kushindwa kueleweka wapo kama kiongozi wa dini unaamua kufanya siasa acha dini pembeni kwanza fanya siasa ukiwa kwenye ibada rudi uongozi wako lakini si kuitia dini kwenye siasa”amesema
Kwa upande wake Katibu mkuu wa ADC ambae ni mjumbe wa umoja huo Doyo Hassan amesema hoja ya kuitisha maandamano ikiwa ni ugumu wa maisha viongozi hao wanapaswa kusaidia wananchi namna ya kukabiliana na hali hiyo ikiwemo kuhamasisha kilimo lakini si maandamano.
Amesema CHADEMA ndio wanufaika namba moja wa 4R za Rais Samia hivyo ni vyema kuziheshimu hizo kwa kuperejesha swala lao kwenye majadiliano ili yapatikane maridhiano ya pamoja.
“Kama kiongozi unapaswa kuwa mstari wa mbele kuwatetea wananchi na kuwasaidia lakini si kuwaingiza kwenye matatizo ya maandamano wao wanarukuzu lakini hakuna hata aliesema ngoja niwasaidie wananchi kwa kuwajengea hata darasa watoto wakasome basi hamasisheni hata kilimo wananchi watumie mvua hizi ili ziwasaidie kupata chakula watajiepusha na njaa”amesema Doyo.
Ameongeza kuwa chama hiko kilisusia kutoa maoni kwenye kikosi kazi lakini pia kwenye baraza hivyo si vyema wao kusema maoni yamepuuzwa wakati watu na makundi yote wametoa maoni yao.
“Haya madai yao ya kusema wapinge maoni ya wananchi yamepuuzwa si ya kweli kila kundi lilifikiwa na likatoa maoni yao sasa kuyapuuza huu ni ubinafsi na kuonyesha wote waliotoa maoni hawana akili jambo ambalo sio sawa”ameongeza Doyo.
Nae Katibu Mkuu wa UDP Saum Rashid amesema utoaji wa maoni ulizingatia makundi yote hivyo kutaka yapuuzwe ni kukwamisha maendeleo ambayo yameonyesha fursa ya usawa wa kijinsia yenye lengo la kufikia 50 kwa 50.
“Huu kwetu wanawake umekuwa mwanga maana tunaona sasa wakati wetu wakushiriki kweny maamuzi umefika sasa hatutakubali mtu yoyote atakaevuruga mchakato huu aidha kwa maslahi ya chama au binafsi”amesema Saum.
Aidha amesisitiza CHADEMA kama ajenda zao ni za msingi ni vyema liitishwe baraza la vyama vya siasa ili kujadili ili nchi iwe salama na si kuitisha maandamano yenye lengo la kuwaumiza wanachi.