Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa New Amani Complex kufuatia ziara maalum ya Wajumbe hao kuangalia Miradi mbalimbali ya Ilani ya Chama hicho Zanzibar.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akiwatolea Maelezo Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC wakati akiwatembeza katika Uwanja wa Kimataifa wa New Amani Complex kufuatia ziara maalum ya Wajumbe hao kuangalia Miradi mbalimbali ya Ilani ya Chama hicho Zanzibar.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akiwa na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC akiwatembeza katika Uwanja wa Kimataifa wa New Amani Complex kufuatia ziara maalum ya Wajumbe hao kuangalia Miradi mbalimbali ya Ilani ya Chama hicho Zanzibar.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC baada ya kuwatembeza katika Uwanja wa Kimataifa wa New Amani Complex kufuatia ziara maalum ya Wajumbe hao kuangalia Miradi mbalimbali ya Ilani ya Chama hicho Zanzibar.
Katibu wa Kamati Maalum Idara ya Itikadi na Uenezi na Mafunzo ya Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC kuhusu Uwanja wa Kimataifa wa New Amani Complex kufuatia ziara maalum ya Wajumbe hao kuangalia Miradi mbalimbali ya Ilani ya Chama hicho Zanzibar.
……..
Na Ali Issa Maelezo .
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Abdull Mwita amesema Uwanja wa New Aman complex tayari umeshakaguliwa na Viongozi wa FIFA na AFCON Kwa matayarisho ya Mashindano AFCON kwa vijana wa chini ya umri wa miaka 17.
Hayo ameyasema leo huko uwanja New Aman Comlex wakati wa mapokezi ya viongozi wa kamati ya NEC ya chama cha Mapinduzi waliofika kiwanjani hapo kufuatia ziara walioifanya kukagua miradi mbali ikiwemo kiwanja cha New Aman Coplex.
Amesema Uwanja huo utatumika kufuatia ushirikiano wa viongozi wa kuu wa Tanzania Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi ambapo kwa sasa Uwanja Huo umeshaamuliwa kutumika kwenye michuano hiyo ambapo tayari viongozi wa FIFA na Viongozi AFCON wameshakikagua na wamejirizisha kufanyika michuano hiyo hapa Zanzibar.
Amesema Zanzibar itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo jambo ambalo ni jema hivyo kuna kila sababu ya kuwapongeza Viongozi wao kwani ni dhahiri kuwa michuano hiyo itasaidia kuwainua vijana kimichezo na kujipatia ajira kutokana na vipaji vyao.
Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbea na Mjumbe wa NEC alishukuru Serikali zote mbili kwa ushirikiano wao kuona kuwa viongozi hao wapo pamoja kwa kushauriana na kupitisha maamuzi ya busara ya pamoja yanayowaletea maendeleo Wananchi.
Amesema wamekuja kujionea wao wenyewe kukagua miradi mbali iliopitishwa katika ilani ya CCM na kuona kuwa viongozi wao wameikamilisha kwa vitendo ikiwa na ubora wa hali ya juu.
Amesema uwanja wa New Amani Coplex upo katika hadhi ya kimataifa na umekidhi viwango vyote vya kimataifa jambo ambalo ni muelekeo wa wazi kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa katika safu ya michezo kushirikisha mashindano mbali mbali ya kimataifa.
Amesema kutokana na hali hiyo hakuna budi kuwashukuru viongozi wao wa kitaifa kuikamilisha ilani ya CCM pamoja na kumshukuru Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na michezo Tabia Abdull Mwita Kwa usimamizi wa Uwanja huo na kumsaidia Rais wa Zanzibar kwa kumpa ushirikiano kwa kila hatua.
Msafara huo wa wajumbe zaidi ya 30 kutoka NEC umetembelea maeneo mbali ya uwanja huo ikiwemo viwanja vya mpira wa mikono, mpira wa miguu na miungombinu mbalimbali ya uwanja huo.