Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mh. Midrik Ramadhan Soraga akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) wametembelea Ofisi ya Uwakilishi Geneva ambapo wamejadili masuala muhimu ya kiutendaji na kidiplomasia. Viongozi hawa wapo nchini Uswisi kwenye ziara ya Makamu wa Rais Mh. Dr. Philip Mpango anayemwakilisha Mh Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) linalofanyika Davos.