Na Mwl. Kassim Mandwanga
Kidatu Kilombero
Asubuhi ya jumatatu Januari 15, 2024, Mh. Dustan Kyobya Mkuu wa wilaya ya Kilombero na mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Kilombero, ameambatana na viongozi kadhaa wa halmashauri katika zoezi la ufunguzi wa shule mpya ya sekondari Lipangalala.
Mh. DC. Kyobya alikuwa ameongozana na Mkurugenzi wa halmashauri Ndugu Zahra Michuzi, Mh Kassim Faya Nakapala mwenyekiti wa halmashauri, Komredi Mwambeleko katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya pamoja na afisa elimu sekondari ndugu Godwin Samson Mukaruka.
Sambamba na ufunguzi huo Mh Kyobya alipanda mti wa kumbukumbu na kusisitiza mambo yafuatayo:
Mh. mkuu wa wilaya amesisitiza kutunzwa kwa miundombinu ya shule hiyo kwa kuwa ndoto ya wana Kilombero ni kuona shule hiyo inakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita.
Katika swala la lishe mkuu wa wilaya amewakumbusha wazazi kizingatia muongozo wa elimu bila malipo kwamba mzazi ana jukumu la kumpatia chakula mtoto, hivyo basi amewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni hapo.
Mh DC, ambaye ni mtu wa vitendo sana, akasisitiza pia majengo yaliyosalia yakamilishwe kabla ya tarehe 22 January 2024.
Sambamba na hilo mwenyekiti wa halmashauri cde Kassim Faya Nakapala ambaye pia ni diwani wa kata ya Lipangalala amemshukuru sana Mh DC na Mkurugenzi kwa utendaji wao wa kazi wa viwango vya juu na kwamba utendaji huo umekuwa chachu ya ukamilikaji wa shule hiyo uliokwama kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu.
Mwenyekiti huyo pia amewashukuru wananchi na kuwataka wanafunzi kusoma Kwa bidii
Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kilombero cde Mwambeleko amewataka wananchi kuwa na imani na Mh Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali yake, pia amewapongeza Mh DC na Mkurugenzi Kwa utendaji wao mzuri pamoja na kuwataka wanafunzi kusoma Kwa bidii.