Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 akiongoza kikao cha kwanza cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar, leo Januari 15, 2024. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulah ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo.