Mabingwa wa Afrika, Timu ya Taifa ya Misri, imeambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya Msumbiji katika mchezo wa kundi B uliochezwa Januari 14, 2024 katika Uwanja wa Stade Félix Houphouët – Boigny nchini Ivory Coast.
Mafarao walianza mchezo kwa bao la mapema kupitia kwa Mostafa Mohamed, akitumia vyema pasi ya Mohamed Salah katika dakika ya 2.
Hata hivyo, katika kipindi cha pili, Witi bila alisawazisha bao hilo dakika ya 55, na dakika tatu tu baadaye, Clésio Baúsque aliipatia Msumbiji bao la kuongoza.
Zikiwa zimeongezwa dakika 11, mshambuliaji wa Misri Salah alifanikiwa kuipatia timu yake bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penati katika dakika ya 90+7.
Mchezo mwengine Ghana ilipoteza baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya timu ya taifa ya Verde Cape
Mtokeo ya mchezo mwengine ni kundi A ambapo timu ya Taifa ya Nigeria ilipata sare ya bao 1 – 1 dhidi ya timu ya taifa ya Equatorial Guinea.