Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Maji, Januari 31 hadi Februari 2, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa chuo hicho, Dk Adam Karia amesema kuwa maadhimisho hayo yatahudhuriwa na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Chuo cha maji kitaadhimisha miaka 50 ya chuo hicho tangu kuanziahwa kwake na kusherehekea mafanikio waliopata.
Mahadhimisho hayo yatafanyika kwa siku tatu Januari 31 hadi Februari 2 mwaka huu