Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 10 Januari, 2024 ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi ya IPU kinachojumuisha Wajumbe kutoka nchi 18 Duniani, kilichofanyika kwa njia ya mtandao.
Viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo utambulisho wa Wajumbe wapya pamoja na kutambua majukumu ya kimsingi ya Kamati hiyo.