Na Issa Mwadangala.
Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali Mkoa wa Songwe wametakiwa kuendelea kujenga ushirikiano na wananchi na kutoa huduma bora ili kujenga imani kwa Wananchi wanaowahudumia.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Poisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya wakati alipofanya baraza na askari wa Mkoa huo Januari 10, 2024 wilayani Mbozi ikiwa ni kufanya tathimini na kuweka mkakati hususani kipindi hiki cha mwaka mpya wa 2024.
Kamanda Mallya pia aliwataka askari Polisi wanapotekeleza majukumu yao kuzingatia weledi na uadilifu ili kuleta matokeo chanya ndani ya Jeshi la Polisi.
Baraza hilo lilifanyika baada ya kufanya ukaguzi na kukagua gwaride kwa lengo la kuangalia utimamu wa askari wa Mkoa wa Songwe.