Kocha wa Kimataifa wa Riadha na aliewahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania – TALGHU, Mzee Jasson Begashe amefariki Dunia usiku wa kuamkia Jumanne tarehe 9 Januari 2024 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Mwanae Sixmund Begashe, Marehemu Mzee Begashe atazikwa siku ya Ijumaa hii tarehe 12 saa nne mchana, Babati Manyara ambapo ndipo alipokuwa akiishi.
Aidha ikumbukwe kuwa Mzee Begashe anamchango mkubwa kwenye tasnia ya Riadha nchini, kwani aliwezesha Taifa kapata heshma kubwa kupitia wanafunzi wake akiwemo mwanariadha wa Kimataifa Juma Ikangaa, John Bura na wengine wengi.
Pamoja na mambo mengine Mzee Begashe mwaka 2010 aikiwa Kaimu Katibu Mkuu waà TALGHU, atakumbukwa kwa ushirikiano wake mzuri na Serikali uliopelekea ongezeko kubwa kwa mishahara ya Watumishi nchini.
Katika Uhifadhi wa Maliasili na Kukuza Utalii nchini, Mzee Begashe alikuwa mmoja wa waasisi wa Marathon kongwe hapa nchini, “Babati Half Marathon”, Mjini Babati iliyovutia wageni wengi kutoka nje ya nchi, na pia kuwa chachu ya marathon nyingi hivi Sasa nchini.
Mzee Begashe atakumbwa zaidi na wakazi wa Babati Manyara kwa kuimarisha michezo, uwasisi wa uwanja wa sasa wa Mpira Mjini Babati, ushiriki wake kwenye mambo ya kijamii nk.