Wahariri na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango wakati akitoa mada kuhusu utekelezaji wa sera mpya ya fedha katika semina iliyofanyika ukumbi wa BoT leo jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu Mwandamizi na Meneja Msaidizi Kurugenzi za Sera, Uchumi na Utafiti Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Lusajo Mwamkemwa akizungumza leo Januaria 9, 2024 Jijini Dar es Salaam kando ya semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa sera mpya ya fedha iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango akitoa mada kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika kikaokazi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam kuelezea mpango wa kuanza kwa utekelezaji wa sera mpya ya Fedha.
……………………………
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuanza kutekeleza sera mpya ya fedha ambayo itatoa fursa kwa wadau wa sekta ya uchumi kuwa na uwelewa mkubwa pamoja na kujua msimamo wa BoT katika kuongeza au kupunguza mzunguko wa fedha katika shughuli za kiuchumi.
Akizungumza leo Januari 9, 2024 Jijini Dar es Salaam kando ya semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari, Mchumi Mkuu Mwandamizi na Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Sera, Uchumi na Utafiti Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Lusajo Mwamkemwa, amesema kuwa mabadiliko ya utekelezaji wa sera ya fedha yamelenga viwango vya riba ambapo nchi mbalimbali Barani Afrika walishaanza kutekeleza.
Bw. Mwamkema amesema kuwa Tanzania imechelewa kutekeleza sera hiyo kutokana kwamba walikuwa wanafanya maandalizi ya kutosha ili kutengeneza mazingira rafiki.
“Mfumo huu sio mpya duniani na sisi Tanzania tunaingia sasa baada ya kujiridhisha kwa kufanya maandalizi ya kutosha, nchi zote za Afrika Mashariki zinaingia katika utekelezaji wa sera hii ili kuwa na ulinganisho wakati watakapoingia katika umoja wa sarafu ya Afrika Mashariki” amesema Bw.Mwamkemwa.
Ameeleza kuwa wana jukumu kubwa la kutoa elimu kuhusu sera ya fedha ambayo BoT wanaelekea kuanza kutekeleza Junuari, 2024.
Bw. Mwamkemwa amesema kuwa wameona ni muhimu kutoa mafunzo kwa wanahabari kutokana na utekelezaji wa sera mpya ambao unaitaji ukaribu na wadau wa uchumi pamoja na wananchi ili kuwa na uwelewa wa maamuzi ya kisera, matarajio pamoja na utekelezaji wake.
“Waandishi wa habari wanajukumu la kufikisha taarifa hizi kwa wananchi na wadau wa uchumi, hivyo tumeuona ni muhimu kuanza na wao ili wapate uwelewa wa ndani kuhusu mabadiliko ya sera ya fedha” amesema Bw. Mwamkemwa.
Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Bi. Vick Msina akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Bw. Lwaga Mwambande akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri kutoka vyombo vya habari wakifuatilia wasilisho la Sera mpya ya fedha inayotarajiwa kuanza kutekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania BoT.
Mchumi Mkuu Mwandamizi na Meneja Msaidizi Kurugenzi za Sera, Uchumi na Utafiti Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Lusajo Mwamkemwa kushoto na Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Bi. Vick Msina wakiwa katika semina hiyo.