NA SABIHA KHAMIS, MAELEZO. 03/01/2024
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban amewataka wanahabari kutoa elimu kwa jamii ili waweze kupata ueelewa kuhusu maonesho ya Biashara.
Wito huo umetolewa huko Nyamanzi Wialaya ya Magharibi “B” katika ukaguzi wa eneo la Mabanda ya maonesho, yanayotarajiwa kufanyika katika Kituo kipya cha kudumu za Biashara, 07junuary 2024.
Amesema maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kila mwaka na mwaka huu, yanarajia kufanyika Nyamanzi,kituo cha maonesho ya Biashara ambacho kimekamilika kwa asilimia isiyopungu 97.
Aidha amesema Mradi huo una Mabanda 9, Ukumbi wa Mikutano pamoja na Vyoo visivyopungua 160 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za Kijamii.
Amefafanua kuwa kutokana na maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar maonesho hayo yatakuwa bila kiingilio (bure) kwa wananchi wote ili kuyaenzi Matunda ya Mapinduzi.
“Ingawa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika eneo hili, Wizara inategemea eneo hili kuwa sehemu ya kujipatia kipato kwa maonesho ya mwaka huu Mhe. Rais ameagiza Wananchi waingie kwenye maonesho bure bila kiingilio” alisema Waziri.
Amewataka Wafanyabiashara wa Daladala hasa wa Nyamanzi kutumia fursa hiyo kujiongezea kipato kwa kuongeza ruti wakati wa maonesho hayo.
Mhe. Omar amesema awamu ya pili ya Ujenzi huo utakuwa na upandaji wa Miti na Nyasi halisi ili kuweka mandhari sawa na hali ya hewa nzuri.
Maonesho hayo ya Biashara ya kila mwaka kwa mwaka huu yanatarajiwa kuanza Tarehe 07 hadi 19 Januari, 2024.
“Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban
Akikagua eneo litakalofanyika maonesho ya biashara yanayotarajiwa kuanza januari 07 -19 2024 huko Nyamanzi wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini magharibi.