Jengo la Soko la Wananchi lililowekewa Jiwe la Msingi na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed (kushoto)akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Soko la Wananchi Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed akimsikiliza Injinia wa Ujenzi wa Halmashauri Mkoa wa Kaskazini Hassan Abdul rahman kuhusiana na Ujenzi wa Soko la Wananchi Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Soko la Wananchi Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji akitoa maelezo ya Kitaalamu kuhusiana na Ujenzi wa Soko la Wananchi Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohamed akitoa hotuba katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la msingi Soko la Wananchi Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja .Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SLIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.31/12/2023)
……..
NA SABIHA KHAMIS MAELEZO
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohamed amewataka Wananchi kutunza Matunda ya Mapinduzi ili yaweze kuwa endelevu kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi Soko la Wananchi wa Mkwajuni amesema Matunda ya Mapinduzi yanahitaji kulindwa kwa maslahi ya Wananchi.
Amesema ni wajibu wa kila Mwananchi kutunza Miradi hiyo ya Maendeleo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kusaidia katika kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Aidha amewataka Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kuzitumia vyema nyezo za uzalishaji wa Mazao jambo ambalo litapelekea kupata Mazao bora na kusaidia Vijana kupata Soko la ajira.
Amesisitiza kuwa mashirikiano ni muhimu katika nchi ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo na kuwa na Taifa imara.
“Kabla ya Mapinduzi Watu walikuwa wanaishi kwa Matabaka hivyo Mapinduzi yamekuja kuondoa Matabaka hayo na kupiga hatua ya maendeleo” alisema Dkt. Khalid.
Aidha amesema Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Dkt. Mwinyi imefanya jitihada kubwa za Maendeleo ikiwemo Ujenzi wa Barabara, Hospital za Wilaya na Mkoa, Skuli za ghorofa na Madiko ya kisasa.
Akitoa Taarifa ya kitaalamu kuhusu Ujenzi wa Soko hilo Katibu Mkuu,Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji amesema Ujenzi wa Soko hilo umegharimu zaidi ya Sh. Milioni 7 na litatumika kwa kufanyabiashara zote ikiwemo Minada ya Mazao mbali mbali.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka Wananchi kulitumia vizuri Soko hilo na kuacha kufanya Biashara katika Mazingira yasio rasmi.
Mradi huo umeanza Ujenzi mwezi machi mwaka 2023 na unatarajiwa kumalizika Mei 2024 ambapo zaidi ya shilingi milioni 300 zimeshatumika katika hatua iliyofikia. Miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar