…………
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Njombe amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima katika Chuo Kikuu cha Zanzibar(SUZA) kwa mchango wake wa kuifungua Zanzibar kiuchumi kupitia utalii na Masoko.
Akizungumza Leo Mwenyekiti huyo Scholastica Kevela amesema kwa hatua hiyo Rais Dk Samia alionyesha anaonyesha na anazidi kuonyesha uhodari wake katika suala zima la uongozi na utalawa ndani na nje ya nchi jambo alililosisitiza kuwa anastahili pongezi.
“Mimi Kama Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe kwa niaba ya wanawake wenzangu wote tunampongeza Rais Samia kwa kuzidi kutuweka juu wanawake jambo linaloashiria wazi kuwa kipawa cha uongozi alichonacho kimetoka kwa Mungu, tunazidi kumuombea ili aweze kufika mbali zaidi” amesisitiza Scolastica
Amesema hiyo siyo shahada ya kwanza ya heshima kutunikiwa kwa Rais Dk Samia hivyo kila mtanzania kwa niaba yake anapaswa kujivunia hilo kwani ni nadra kutokea kwa viongozi Duniani kote
“Wanawake wa Tanzania tulishamua kumuunga mkono kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali mwakani na ule uchaguzi Mkuu Mwaka 2025 tukiwa na uhakika wazi kuwa CCM itaibuka na Ushindi wa kishindo” amesema Scolastica
Katika Hafla ya Mahafali hayo ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu tarehe 28 Desemba, 2023., Samia Samia alieleza wazi hatua alizopitia katika historia yake huku akimpongeza Rais Mstaafu Dk Amani Abeid Karume kwa kumnoa katika uongozi.
Mbali hayo na kiongozi huyo Rais Dk Samia Suluhu Hassan hakuacha kuwapongeza viongozi mbalimbali aliofanya nao kazi katika awamu mbalimbali ndani ya Serikali hiyo ya Zanzibar hadi kufanikiwa kuanzishwa kwa chuo hicho cha SUZA miaka 19 iliyopita
Akizungumzia hayo Mama Kevela amesema Taifa la Tanzania na visiwa vyake linajivunia kazi nzuri ya Rais Samia huku akisisitiza kuwa wao Kama wanawake wa Taifa hili hususani kutoka Chama Cha Mapinduzi watamuunga mkono wakati wote.
Aidha akizungumza katika mahafali hayo Rais Dk Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake wote nchini kuleta mabadaririko chanya mara pale wanahitimu elimu katika vyuo mbalimbali.
Amesema amefarijika kwa kiasi kikubwa kuona asilimia 58 ya waliofanya vizuri katika mtihani wao chuoni hapo ni wanawake jambo alililowataka kuongeza juhudi.
Aidha kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan hiyo ni PhD ya tatu kutunukiwa tangu awe Rais wa Tanzania ya kwanza alitunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya SUZA amekabidhiwa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi.
Pia hivi karibuni Rais Dk Hassan alitunukiwa Udaktari wa heshima (PhD) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Udaktari wa heshima (PhD) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (JNU) cha nchini India.