Picha no.DSC-0028-MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla,akihutubia mamia ya Vijana wa UVCCM katika ufunguzi wa Matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofanyika Uwanja wa Makontena Wilaya ya Mkoani Pemba.
……………
NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Mhe.Hemed Suleiman Abdulla,amesema CCM ndio Chama pekee chenye hadhi ya kuendelea kuongoza Serikali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo aliitoa wakati akifungua Matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, yaliyozinduliwa Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Makontena.
Mhe.Hemed,amefafanua kuwa hakuna chama kingine cha siasa nchini kinachoweza kuwa mbadala wa CCM kwa sasa na miaka mingi ijayo.
Katika maelezo yake Mhe.Hemed,alieleza kuwa Chama hicho na Jumuiya zake hasa UVCCM kinaimarisha Sera zake ziendane na mahitaji halisi ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar.
“Tutaeleza kwa nidhamu na unyenyekevu mkubwa kwa wananchi na tunayo nafasi pia ya kuwaeleza wale vijana wenzenu ambao wapo katika upande ambao sio sahihi waelezeni mambo mema yanayofanywa na Serikali kupitia Rais Dk.Mwinyi na Rais Dkt,Samia wanaendelea kutekeleza vyema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.”,alisema Mhe.Hemed.
Akifafanua baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa katika miundombinu ya ujenzi wa barabara alisema hivi karibuni serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara kilomita 277 huko nyuma zipo kilomita 275.9 za vijijini kulikuwa na mkataba wa kilomita 100.9 za mijini.
Amesema katika maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi itazinduliwa miradi 160 ambayo ni idadi kubwa kuliko miaka mingine.
Aliwataka viongozi wa UVCCM kwenda kusimamia nidhamu ya taasisi kwani baadhi ya vijana wanatumia migongo ya viongozi wa juu kujinufaisha na kufanya mambo yasiyofaa na kuwataka kuondosha majungu na kufanya kazi za jumuiya.
Alisema viongozi hao wamekaa na kusema kuwa bado wanayo nafasi ya kuongeza fursa za vijana kupitia Serikali na sekta binafsi ili wanufaike.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed Ali Kawaida, alisema msimamo wa Umoja huo ni kuhakikisha Rais Dk.Mwinyi na Rais Dkt.Samia wanapata ushindi mkubwa mwaka 2025.
Mapema akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis, alisema Vijana wana wajibu wa kulinda kwa vitendo Mapinduzi kwani yalifanywa na Vijana wa wakati huo kupitia Kamati Maalum ya Watu 14 wakiongozwa na aliyekuwa Rais wa kwanza Marehemu Abeid Aman Karume,
Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi,alieleza Vijna hao waendelea kuyaenzi na kuyaishi Mapinduzi kwa kuunga mkono fursa na mipango ya kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor,alisema Serikali imeboresha miundombinu ya barabara kwa kilomita 166.6 utakaojengwa hivi karibuni na kujumuisha barabara 18.