Hifadhi ya Taifa Arusha imemtuza Cheti cha pongezi Bwana Josephat Matemu kama sehemu ya kutambua juhudi zake thabiti za kutembelea Hifadhi hiyo kwa takribani miaka 15 mfululizo, hafla ya kumkabidhi Cheti hicho ilifanyika tarehe 26/12/2023 katika ofisi za Hifadhi ya Taifa Arusha.
Ndugu Matemu ni mkazi wa Arusha, amekuwa na desturi ya kutembelea Hifadhi ya Taifa Arusha na kulala katika malazi yaliyojengwa na TANAPA (Rest House) na amekuwa akifurahia huduma zinazotolewa na Hifadhi na kupelekea kupaita kuwa Hifadhi ni Nyumbani “(Arusha National Park is our Second Home)”
Ndugu Mtemu, amekuwa akitembelea Hifadhi hiyo yeye na familia yake katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kuanzia mwaka 2008 hadi 2023.