Waziri wa Uchumi wa buluu na uvuvi Mhe. Suleiman Masoud Makame akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha wajasiriamali Hanyegwa mchana ikiwa ni shamrahamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi.
Waziri wa Uchumi wa buluu na uvuvi Mhe. Suleiman Masoud Makame akitembelea nakukagua mabanda katika kituo cha wajasiriamali Hanyegwa mchana mara baada ya kukifungua ikiwa ni shamrahamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi.
Katibu Mkuu (OR),tawala za mikoa,serikali za mitaa,na idara maalum za SMZ Issa Mahfudhi Haji akitoa maelezo ya kitaalamu kuhusiana na ujenzi wa kituo cha wajasiriamali (karakana) kilichogharimu shilingi bil.1na milioni mia tisa hadi kukamilika kwake na kuwa na uwezo wa kuchukua wajasiriamali 300,hukomhanyegwa mchana Wilaya ya kati Unguja.
Waziri wa Uchumi wa buluu na uvuvi Mhe. Suleiman Masoud Makame akihutubia mara baada ya kuzindua kituo cha wajasiriamali (karakana) kilichogharimu shilingi bil.1na milioni mia tisa hadi kukamilika kwake na kuwa na uwezo wa kuchukua wajasiriamali 300,hukomhanyegwa mchana Wilaya ya kati Unguja.
Maafisa na watendaji wa kikosi cha zimamoto wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa kituo cha wajasiriamali (karakana) kilichogharimu shilingi bil.1na milioni mia tisa hadi kukamilika kwake na kuwa na uwezo wa kuchukua wajasiriamali 300,hukomhanyegwa mchana Wilaya ya kati Unguja. (PICHA NA FAUZIA- MAELEZO ZANZIBAR)
……
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Suleiman Masuod Makame amewataka wajasiriamali wa Wilaya ya Kati na maeneo jirani kulitumia vyema eneo la karakana ili kuendelea kuwaunganisha pamoja .
Hayo ameyasema leo huko Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa uzinduzi wa karakana hiyo kuelekea kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Amesema jengo hilo limejengwa kwa fedha za mfuko wa ahueni ya uviko 19 na liko tayari kutumiwa na wajasiriamali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hiyo na vitongoji vyake.
Aidha Waziri huyo aliwataka wananchi hao kuunga mkono juhudi zinazochukiliwa na viongozi wao na kuzichangamkia frusa zitakazowaondolea changamoto za maisha.
‘Nawaomba wajasiriamali watakaopata nafasi katika jengo hili mlitumie jengo kwa vizuri na mlifanyie usafi na kulitunza kwa maslahi yenu, ya kizazi kijacho na Taifa kwa ujumla” alisisitiza Waziri Masoud
Pia, aliwataka wananchi hao kulipia tozo zitakazowekwa kwani fedha hizo ndio zinazoenda kutumika kwa mahitaji mbalimbali ya jengo hilo ikiwemo malipo ya maji, gharama za umeme ulinzi na gharama nyengine mara baada ya kumalizika kwa muda waliopewa kufanya kazi zao katika eneo hilo bila malipo.
Akitoa taarifa ya kitaalamu Katibu mkuu ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikala za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahfudhi Haji alisema karakana hiyo imejengwa na kisoksi cha Zimamoto ambapo ujenzi huo ni wenye viwango na kukidhi mahitaji yaliyotakiwa.
Afahamisha kua jumla yawajasiriamali 300 wataweza kufanya kazi mbalimbali katika karakana hiyo ikiwemo utengenezaji wa vyombo vya moto wafanya biashara za mbao, ufundi seremala na wauzaji wa bidhaa nyengine kwa wakati mmoja.
Akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Ayuob Mohammed Mahamud alisema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuzalisha ajira kwa vijana na kuwataka vijana kujitokeza kuiikimbilia fursa hiyo.
Hata hivyo aliishauri Mkurgenzi wa Manispaa ya Wilaya ya Kati kuweka kipaombele kwa maombi ya wazawa na wakaazi wa Wilaya hiyo kuweza kupata nafasi katika jengo hilo.
Mradi huo umekamikika ukiwa na Bloki 9 za maeneo ya kufanyia kazi na biashara na umegharimu jumla ya shillingi Bilioni Moja na Milioni 900 za kitanzania.