Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani akizungumza na vyombo vya habari.
Na. Zillipa Joseph, Katavi.
Ni wakati wa sherehe za krismasi ambapo wakristo duniani kote wanaungana na wakristo wenzao kusheheherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkombozi wao Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Katika sherehe hiyo kama illiyo kwa sherehe zingine, watu wazima wamekuwa na desturi ya kwenda kutembelea maeneo mbalimbali ya starehe, na wengine wakiandamana na watoto wao.
Katika sherehe za mwaka huu wazazi na walezi wanashauriwa kuwaacha watoto wao hasa wenye umri wa chini ya miaka nane katika uangalizi salama.
Tunaposema uangalizi salama tunawalenga wale wazazi wenye tabia ya kuwaacha watoto nyumbani bila ya kuwepo kwa mtu mzima, kuhakikisha wanawaacha na mtu mwenye akili timamu ili kuwalinda na ajali zozote ambazo zingeweza kuzuilika..
Aidha wapo wazazi/walezi wanaowapa fedha watoto wakatembee peke yao bila mtu mzima hali inayoweza kusababisha ajali barabarani.
Kufuatia hali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani amewakumbusha wazazi /walezi kuacha kuwapeleka watoto katika kumbi za starehe maarufu Kama disco Toto..
Aidha kamanda Ngonyani amesisitiza wazazi wanaowaacha watoto nyumbani wahakikishe kuna uangalizi wa mtu mzima.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi walioulizwa kuhusu suala kuwaacha watoto wakatembee peke yao wamesema huo sio utaratibu mzuri kwani wakati wa sikukuu watu wengi wanalewa na wanakosa umakini.
Nao watoto walioongea na mwandishi wa habari hii walikuwa na maoni tofauti ambapo wao walidai sikukuu nzuri ni ile yenye chakula.kitamu, nguo mpya na hela ya kwenda kutembea.
Walipoulizwa zaidi juu ya matembezi yao walisema wakifika mjini wananunua vitu mbalimbali na kula na kuongeza kuwa kama wana fedha za kutosha wanakwenda kuogelea katika sehemu za starehe.