Makamu wa Pili wa Rais  Mstaafu  (SMZ) Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo jipya la maabara ya kisasa ya wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi (ZFDA)  huko  Mombasa ikiwa NI miongoni mwa  shamrashamra  za maadhimisho ya miaka 60  ya Mapinduzi ya Zanzibar.

…………………….. 

Makamu wa Pili wa Rais  Mstaafu Mhe. Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi kutumia vyakula na dawa zenye kiwango ili kuzilinda Afya zao.

Akifunguwa Jengo la Maabara ya Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar ZFDA huko  Mombasa Wilaya ya Magharibi ‘B’.ikiwa ni miongoni mwa  Shamra Shamra  za Maadhimisho ya miaka 60  ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema utumiaji wa dawa na vyakula ambavyo havina kiwango vitasababisha madhara ya kiafya  kwa mtumiaji na kuipatia  hasara Serikali kwa  kutoa gharama kubwa ya matibabu

Aliwataka wafanyakazi wa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi kuvitunza vifaa vya maabara walivyowekea pamoja na kutoa huduma kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Mhe.Balozi aliwafahamisha kwamba waendeleze kudumisha nidhamu wakati wa  kazi ili kuwa na bidii uhakika na haki bila ya kumuonea mfanyabiashara yeyote Jambo ambalo litaongeza ufanisi wa majukumu yao.

Nae Waziri wa Afya Mhe. Nassour Ahmed Mazrui amesema maabara imejengwa kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa ambayo vitachunguza dawa na vyakula pamoja na bidhaa  zinazozalishwa ndani na nje ya nchi ili kuona ubora na usalama wa bidhaa hizo 

Alieleza kuwa Wawekezaji wanaokuja kuekeza bidhaa za vyakula na viwanda wataridhika kuona maabara yenye hadhi kubwa ya kimataifa .

Mapema Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Chakula  Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA)  Burhan Othman  amesema  kukamilika Kwa maabara hiyo kutasaidia kuengeza  nyanja za uchunguzi  ambapo awali kulikuwa hakuna  uwezo huo, pamoja na kurahisisha mzunguko kwa wafanyabiashara .

Amesema jengo la maabara ya ZFDA ni la Kwanza kwa hapa Zanzibar na lina ghorofa tatu  zimejengwa  kupitia pesa za mradi wa maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  katika awamu mbili ya kwanza mradi ulitumia Tshs Bilioni 5.4 Kwa ajili ya jengo na Bilioni 4.4 Kwa ajili ya vifaa.

Ujenzi huo ulianza Machi 2019 na kukamilika Juni 2022 na mchakato wa manunuzi ya vifaa vya maabara hiyo ulianza Julai 2022 na kukamilika Disemba 2023.