Na Meleka Kulwa-Fullshangwe Blog, Dodoma
Mzee Kayumba, mkazi wa Dodoma, amefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) pamoja na bidhaa zinazotengenezwa na mamlaka hiyo, akibainisha kuwa vijana wa Kitanzania wanafanya kazi kubwa yenye ubora unaovutia.
Amesema hayo Juni 19, 2026 alipotembelea banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Amebainisha kuwa amefurahishwa na vifaa vinavyotengenezwa na VETA, akisema vinaonyesha ubunifu mkubwa wa vijana wa Kitanzania na kwamba vinapendeza.
Aidha, amesema kuwa VETA inapaswa kuendelea kuwajengea uwezo vijana katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali, akibainisha kuwa maendeleo ya nchi yanaweza kupatikana kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.
Pia ameongeza kuwa bidhaa zinazotengenezwa na vijana wa Kitanzania ni bora, na kwamba Watanzania wanapaswa kuzithamini na kuzitumia.
Aidha, ametoa wito kwa vijana na wazazi kutembelea mabanda ya VETA ili kujifunza fursa zilizopo, huku akiwahimiza vijana kujiunga na vyuo vya ufundi ili kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.
