Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) amekabidhi magari 5 kwa Mkoa wa Dodoma kwa kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za Afya.
Akikabidhi magari hayo Waziri Mchengerwa amewataka waganga wakuu wa Halmashauri za mkoa wa dodoma kuzitumia gari hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili ziweze kusaidia wananchi.
“Mhe. Rais ametoa gari hizi kwa watanzania, mpango wa Serikali ni kila Halmashauri ipate gari moja ya shughuli za usimamizi na kila Jimbo la Uchaguzi lipate gari moja ya kubebea wagonjwa. Mpaka sasa kwenye mkoa wa Dodoma mmeshapokea magari 3 kwenye Halmashauri za Mpwapwa, Chamwino na kwenye Hospitali ya Afya ya Akili Milembe na leo halmashauri zingine zinapata gari kwa ajili ya usimamizi
“Gari hizi zitumike kwa lengo lililokususiwa kwani ni maono ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndio maana ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa magari haya. takribani shilingi Bilioni 52 zimetolewa kwa ajili ya kunua magari 528 kati ya hizo gari 316 ni za kubebea wagonjwa na nyingine 212 ni kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za Afya kwenye Mikoa na Halmashauri zote nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemarry Senyamule amemshkuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassankwa kutoa gari hizo kwa Mkoa wa Dodoma kwani zitasaidia utoaji wa huduma za afya.