Na Sophia Kingimali,Dar es salaam.
Chama cha Mapinduzi CCM kimelitaka Shirika la Umeme TANESCO kutatua changamoto ya umeme kwa wananchi kwani imeshakuwa kero na kukwamisha maendeleo kwa kuwarudisha nyuma wafanyabiashara wadogo kama vinyozi na wengine ambao kipato chao kikubwa kinategemea umeme.
Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 21,2023 Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda amesema changamoto ya umeme inapaswa kutatuliwa kwani wananchi wengi wamekua wakilalamikia hali hiyo ambayo imeshakua kero miongoni mwa watanzania.
“Niwaombe watendaji wa TANESCO mtoe taarifa ya tatizo la umeme mkiwa site ambapo wananchi watawaona na kuwaelewa lakini si kukaa ofisini na kutoa taarifa wananchi wanataka kuona kama mnashughulikia wanaona kweli kazi inafanyika”amesema Makonda.
Aidha Makonda amewataka kujitathmini kama watendaji ambao wamewekwa kumsaidia Rais kama wanatimiza majukumu yao ili kutimiza adhma yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Chama cha Mapinduzi kinaona changamoto hiyo ya umeme na hapo lazima waseme ukweli hasa Kwa watendaji wa Shirika la Umeme nchini TANESCO kujitathimini kwani haiwezikani Mwenyekiti hadi analazimika kuvunja Bodi kwasababu uwajibikaji mdogo wa watendaji hivyo hata watendaji wa TANESCO kama wameshindwa basi wanatakiwa kujipima”amesema.
“Sisi sote tunaishi huko mtaani na tunaona tatizo hili lilivyo kubwa na ndio maana Mimi Kila siku nasema kuwa nitasema kweli daima na hapa lazima TANESCO wajipime kwani mara nyingi hatua zinachukuliwa Kwa wanasiasa tu na hivi tutaangalia na uwajibikaji wa watendaji wetu.”amessitiza
Ameongeza kuwa watendaji wote wa taasisi za umma wakiwemo TANESCO wajitathimini kwani Rais amewaweka hapo walipo ili waweze kumuwakilisha katika kuwahudumia wananchi