Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku mmoja wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya Arobaini na Tisa Duru ya Pili na ya Tatu.Mahafali hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Mh.Jaji Damian Lubuva wakati wa Mahafali ya Arobaini na Tisa Duru ya Pili na ya Tatu.Mahafali hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho katika Mahafali ya Arobaini na Tisa Duru ya Pili na ya Tatu.Mahafali hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiingia katika Ukumbi wa Mlimani City kwaajili ya Sherehe za Mahafali ya Arobaini na Tisa Duru ya Pili na ya Tatu.Mahafali hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika Ukumbi wa Mlimani City katika Mahafali ya Arobaini na Tisa Duru ya Pili na ya Tatu.
*******************************
EMMANUEL MBATILO
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imeitaka Serikali kushughulikia changamoto wanazozikabili ikiwemo uhaba wa wafanyakazi ,wanataaluma na waendeshaji.
Akizungumza katika Mahafali ya 49 Duru ys Pili na ya Tatu, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mh.Jaji Damian Lubuva ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa pesa za kuimarisha miundombinu katika maeneo mbalimbali chuoni hivyo ameitaka iendelee kushughulikia changamoto zinazowakabili.
“Serikali imekipatia chuo fedha kwaajili ya ukarabati wa ndaki ya Uhandisi na Teknoloji, nyumba za wanafanyakazi na mabweni ya wanafunzi.Baraza lilifurahishwa sana na hatua ya Serikali kuanza kulipa fedha za madai ya wafanyakazi ikiwemo posho ya nyumbani,malimbikizo ya mishahara, kiinua mgongo na madai mengine”. Amesema Mh.Jaji Lubuva.
Aidha Mh.Jaji Lubuva amesema kuwa watasimamia kwa ukamilifu fedha zote zinazotolewa na Serikali na zile zinazopatikana kutoka vyanzo vya ndani vya mapato ya Chuo.
“Nasi kwa upande wetu tunamuahidi Mheshimiwa Rais na Serikali yake kwamba tutaendelea kusimamia na kudumisha ubora wa elimu hapa Chuoni kwa kuhakikisha kuwa sheria,kanuni na taratibu zinazingatiwa”. Ameongeza Mh.Jaji Lubuva.
Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye amesema kuwa maendelea ya Chuo tangu Mahafali yaliyopita ya 48 yakiwemo kuimarisha ulinzi na usalama hasa kwa kuongeza taa za barabarani na kukarabati zilizopo, na kufunga kamera za usama kwenye maegesho ya magari.
Pamoja na hayo amesema kuwa kumekamilika ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,009 kwa mara moja katika chuo kishirikishi cha Elimu Mkwawa, Jengo hilo pia lina madarasa matatu yanayoweza kuchukua wanafunzi 200 na ofisi zitakazotumiwa na wahadhiri 28.
Wahitimu wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanajijengea utamaduni wa kujiajili kutokana na hali ya ajira kuwa ngumu nchini, hivyo wao wamejifunza mambo mengi vyuoni hivyo kwao itakuwa rahisi kujijengea kujiajiri