Home Mchanganyiko BITEKO ANG’AKA KUHUSU MISHAHARA YA WATANZANIA MIGODINI

BITEKO ANG’AKA KUHUSU MISHAHARA YA WATANZANIA MIGODINI

0

Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Richard Jordonson wa tatu kulia
akimuonyesha kitu Waziri wa Madini Doto Biteko wa pili kushoto.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel na kushoto Makamu
Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Simon Shayo wakati wa ziara ya
Waziri wa Madini mgodini hapo.

Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akiwa kwenye kikao na uongozi
wa mgodi wa dhahabu wa Geita “GGM” wakati wa ziara yake mgodini
hapo. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu
wa Wilaya Joseph Maganga na kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi
Mtendaji wa GGM Richard Jordonson.

**************************************

Na Issa Mtuwa – Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko pamoja na kuupongeza uongozi wa mgodi
wa dhahabu wa Geita “GGM” katika mambo mengi leo tarehe 16/11/2019
alikuwa “mbogo” kwa uongozi huo kuhusu suala la mishahara wanayolipwa
Watanzania ambapo amebaini kutokuwepo kwa usawa.

Biteko amesema anaumizwa sana na jambo la malipo ya mishahara kati ya
Watanzania na wageni licha ya kulingana kwa sifa, ujuzi na elimu na wakati
mwingine mtazania anasifa zaidi kuliko mgeni lakini bado mtanzania
analipwa chini kuliko yule mgeni.

Kutokana na hali hiyo, Biteko ameuagiza uongozi wa GGM kuwasilisha
orodha ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi wote (Payroll) kwa
Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa wiki ijayo. Biteko alianza
kuhoji idadi ya idara zilizopo na zinaongozwa na akina nani huku akiuliza
kuna watu wangapi wa kigeni katika idara hizo na majukumu yako.

“Sheria ya madini hasa sheria ya Local content inatoa muongozo ni namna
gani na wakati gani mgodi unaweza kumuajiri mtaalamu wa fani fulani
kutoka nje endapo hakuna mtanzania wa kuweza kushika wadhifa huo”
amesema Biteko.

Ameongea hayo wakati akiongea na uongozi wa mgodi wa GGM mkoani
geita alipotembelea mgodini hapo kwa ziara maalum ya kikazi kwa lengo la
kufuatilia na kukagua uendeshaji wa shughuli za mgodi huo, ufuatilia na
kuangalia utekelezaji wa malalamiko ya wananchi na malipo ya ushuru wa
Halmashauri (Service Levy) ambapo mgodi huo unawajibika katika malipo
hayo.

Aidha, Biteko amekwenda kujiridhishi katika masuala mbalimbali ambayo
kamati maalumu aliyoiunda kwenda mgodini hapo kwa ajili ya kuangalia na
kukagua ili ajiridhishe kabla ya kutoa idhini ya kuruhusu mgodi huo kuanza
uchimbaji wa chini kwa chini (Underground) kufuatia maombi ya mgodi huo
kwa waziri.

Kwa mujibu wa kifungu cha 40 cha marekebisho ya sheria ya madini ya
mwaka 2017 hairuhusu uchimbaji wa chini kwa chini kwa mwekezaji au
mgodi mpaka apate idhini (Kibali) ya waziri mwenye dhamana ya Madini
ambapo Waziri alianisha mambo mengi ya kuzingatiwa na mgodi kabla
hawajaruhusiwa.

Biteko ameendelea kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kuwa raslimali
hizi ziwe neema kwa wananchi na sio mateso. Kauli hiyo ameitoa kufuatia
malalamiko ya wananchi wapatao 350 ambao makazi yao yalipitiwa na
tetemeko wakati wa milipuko mbalimbali mgodini hapo wakati wa ulipuaji
wa miamba.

Ameongeza kuwa hadi kufikia mwisho mwaka huu ukurasa wa suala la
malipo ya fidia ya suala hili liwe limefungwa na kwamba wenye malalamiko
wote wapeleke kwa Mkuu wa Wilaya Geita kuanzia tarehe 18-23/11/2019.

Kwa upande wa uongozi wa mgodi ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji
wa Mgodi Richard Jordanson na Makamu Mkurugenzi Mtendaji Simon
Shayo kwa nyakati tofauti wametoa shukrani kwa ujio wa Waziri kwenye
mgodi wao ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea tangu alipoteuliwa
kuwa Waziri wa Madini.

Wameongeza kuwa mgodi wao upo mstari wa mbele kutekeleza maagizo
ya serikali na kwamba wanapenda kuwa msistari mbele na wawe wa
kwanza katika kuchangia sehemu kubwa itakayo changia pato (GDP) la
taifa kwa upande wa madini.

Shayo amemwambia waziri kuwa mambo mengi aliyoyasema Waziri kama
vile; mpango wa ufukiaji mashimo baada ya mgodi kufungwa, ulipaji wa
ushuru wa Halmashauri za wilaya (Service levy), mchakato wa ulipaji wa
fidia ya wananchi na utekelezaji wa sheria ya local content vinatekelezwa
baadhi vimeshakamilishwa na baadhi vipo kwenye taratibu za kukamishwa.

Akiwa kwenye mgodi wa RZ unaomilikiwa na mwekezaji kutoka china anae
fahamika kwa jina la “Lyuu” amemtaka mwekezaji huyo kwa kufanya kazi
zake kwa kuzingatia sheria zote zikiwemo za madini, kazi na utoaji wa
mikataba ya ajira na makato ya NSSF kwa wafanyakazi wake na
kuiwasilisha kwa mamlaka husika.

“Lyuu” amesema ameshukuru waziri kutembelea mgodi kwake na
amepokea maelekezo ambayo ameyakubali na kuahidi kuyatekeleza.
Wakati wakati huo huo wafanayakazi walipo mgodini hapo amewataka
kuwa waaminifu na kuepuka vitendo vihovu kwa mwekezaji.