Na Sophia Kingimali,Dar es salaam
Serikali imesema itaendelea kushirikiana na TAMSTOA ili kuhakikisha inaendelea kuleta maendeleo na mchango kwa uchumi wa nchi huku akiwataka madereva na wamiliki wa Maroli kufuata seheria.
Hayo yameelewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Barabara Bw. Andrew Magombana akimuwalilisha Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi kwenye mkutano wa nne wa mwaka ya Chama cha Wamiliki wa Maroli (TAMSTOA).
Amesema serikali inasaidia kutatua changamoto mbalimbali ili kuhakikisha uwekezaji wao unarudi katika fedha walizowekeza.
“Sisi kama wizara ya uchukuzi ni kama kiunganishi kwa hiyo tutakaa na wenzetu wa TARURA,TANROAD na wadau wa mikoani ili kuhakikisha changamoto zinatatuliwa”amesema.
Akizungumizia ajira kwa madereva amesema madereva wanapaswa kuisoma sheria na kuielewa ili iweze kuwasaidia kupata stahiki zao na pia waweze kufanya kazi zao kwa utulivu na kufuata sheria ili kuepuka ajali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Maroli (TAMSTOA) Bw. Chuki Shabani pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanaishukuru serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano pindi linapotokea tatizo.
Amesema sekta ya usafirishaji ni sekta ya pili nchini kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni.
Sambamba na hayo Shabani amewataka wamiliki wa maroli ambao hawajajiunga na vyama hivyo kujiunga ili kuwa na kauli moja pindi serikali inapotoa maagizo kuhusu sekta hiyo
“Hili swala la mikataba lipo kisheria na ndio maana tunatamani hawa ambao hawapo kwenye vyama mbalimbali ili isaidie serikali.inapotoa agizo liweze kutekelezwa na watu wote maana hata swala la miktaba asilimia kubwa linatekelezwa na wale walio kwenye vyama ambao hawapo ndio hizo changamoto ambazo zinaelezwa hasa za kutowapa mikataba madereva maslahi yao mengine”amesema.
Nae,mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Masafa Marefu Tanzania Hassan Dede amewataka wamiliki kuzingatia maslahi ya dereva awapo kazini ili kuleta motisha katika utendaji kazi yake.
Amesema madereva wamekua wakipitia changamoto kubwa hali inayopelekea kufanya kazi kwa mawazo na mwishowe kutoka nje ya maadili yao ya kazi.
“Waajiri wanapaswa kututhamini sisi kama madereva ili tuweze kufanya kazi zetu kwa umakini katika kuepusha ajali pia wizi unaofanywa na baadhi kwa kuchukua mafuta kwenye matanki na wengine kuuza matairi na wanafanya hivyo kutokana na kazi kubwa wanayoifanya lakini hawana maslahi nayo”amesema Dede.