Mtendaji wa Kijiji cha Msimbazi wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe Bi. Matilda Modestus Mwapinga akizungumza na wahariri wa Habari waliofika katika kijiji hicho kwa ajili ya kukagua miradi ya madarasa ya shule na nyumba za walimu inayotekelezwa na TASAF katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa kijiji cha Msimbazi
Raphael Michael Madati akizungumzia umuhimu wa ujenzi wa madarasa hayo na nyumba za walimu katika kijiji cha Msimbazi.
Mwalimu wa Taaluma Shule ya Msingi Mzimbazi Arafat Mtolela akiishukuru serikali kupitia TASAF kwa ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu.
………………………..
NA JOHN BUKUKU, NJOMBE.
Uongozi wa Kijiji cha Msimbazi Mkoa wa Njombe wameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kutoa shilingi milioni 260 kwa ajili ujenzi wa madarasa manne pamoja na nyumba za walimu jambo ambalo limeokoa watoto wao waliokuwa katika hatari ya kukosa elimu kwani awali wanafunzi katika Kijiji hicho walikuwa wanapata adha na kutembea umbali mrefu kwenda Shule.
Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari leo Desemba 20, 2023 wakati walipotembelea mradi wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa na nyumba za walimu zilizojengwa na TASAF katika Kijiji cha Msimbazi Mkoa wa Njombe.
Mtendaji wa Kijiji cha Msimbazi Matilda Modestus Mwapinga, amesema kuwa mwaka 2017 walianza kupokea fedha ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ajili utekelezaji wa mradi wa madarasa mawili pamoja na matundu ya choo.
Mwapinga amesema kuwa katika mradi huo TASAF walitoa shilingi milioni 65 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi, huku wanakijiji wakitakiwa kuchangia asilimia 10 katika kufanikisha mradi huo.
“Tulifanikiwa kutekeleza mradi wa madarasa kwa msaada wa TASAF jambo ambalo limeleta tija katika maendeleo ya kijiji” amesema
Mwapinga.
Amesema kuwa mwaka 2018 TASAF waliweza kuwapatia mradi mwingine wa Nyuma za walimu pamoja na madarasa.
“Pia mwaka 2020 tulipata mradi wa ujenzi wa darasa moja kwa ajili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki” amesema
Mwapinga.
Mwenyekiti wa kijiji cha Msimbazi
Raphael Michael Madati , ameipongeza TASAF kwa kutoa fedha za ujenzi ya Madarasa kwani imewasaidia wanafunzi kutokana awali wanakuwa wanatembea umbali mrefu Kilometa 4.5 kwa ajili ya masomo.
Mwalimu wa Taaluma Shule ya Msingi Mzimbazi Arafat Mtolela, ameishukuru TASAF kwa ushirikiano waliotoa katika kufanikisha ujenzi madarasa na ujenzi wa choo.
Amesema kuwa shule ya Msingi Mzimbazi inajumla ya wanafunzi 185 ambayo idadi hiyo ni wengi ukilingani na idadi ya Madarasa yaliopo.
“Uhitaji wa madarasa bado ni mkubwa , hivyo tunasubiri fedha kutoka serikalini ili tuongeze madarasa kwani kwa sasa darasa la kwanza na pili wanasoma katika darasa moja kwa kupeana zamu” amesema
Mtolela.
Ameeleza kuwa pia wanaupungufu wa nyumba za walimu kutokana kuwa kwa sasa kuna walimu watano na nyumba zilizopo ni manne.
Baadhi ya wahariri wa habari wakiwa katika moja ya madarasa yaliyojengwa na TASAF katika kijiji cha Msimbazi.
Baadhi ya madarasa na nyumba na walimu zilizojengwa na TASAF katika kijiji cha Msimbazi.