Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Masaburi akizungumza na Wafanyabiasha wa Soko la Temeke Sterio leo Desemba 19, 2023 akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wafanyabiashara wakiwemo Mama Lishe katika Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Masaburi akiwa katika picha ya pamoja na Mama lishe wakati akitoa msaada wa majiko ya Gesi kwa Mama Lishe katika Soko la Temeke Sterio, Tandika, na Keko kwa ajili ya kuwakumbusha umuhimu wa matumizi nishati mbadala katika utunzaji wa mazingira.
Diwani wa Viti Maalum Caroline Henrich akizungumza jambo wakati Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Masaburi alipofanya ziara katika Soko la Keko.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Masaburi akizungumza na Wafanyabiasha wa Soko la Temeke Sterio leo Desemba 19, 2023 akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wafanyabiashara wakiwemo Mama Lishe katika Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam (Picha na Noel Rukanuga)
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Masaburi amewata wafanyabiashara wakiwemo Mama Lishe katika Soko la Temeke Sterio, Tandika na Keko kutunza mazingira pamoja na kutumia nishati mbadala katika utekeleza wa mjukumu yao jambo ambalo litasaidia kuzuia mabadiliko ya Tabia ya Nchi ambayo yanasabishwa na kutaji wa miti.
Akizungumza na Wafanabiashara wa Soko la Temeke Sterio, Tandika na Keko kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wafanyabiashara iliyofanyika leo Desemba 19, 2023, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Masaburi, amesema kuwa wakati umefika kwa mama lishe kuacha kutumia mkaa pamoja na kuni badala yake wanapaswa kutumia gasi.
Mhe. Masaburi amesema kuwa matumizi ya gasi ni rafiki katika kuhakikisha tunatunza mazingira yetu pamoja na kujiepusha na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.
“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ametuagiza tuje kutoa elimu hii ili kuhakikisha tunatumia nishati mbadala katika matumizi yetu ya kila siku” amesema Mhe. Masaburi.
Mhe. Masaburi amewakumbusha wanawake kuacha kuchukua mikopo ya kausha damu badala yake wakope mikopo inayotambulika na Serikali ikiwemo taasisi za fedha.
“Nawaomba wanawake wenzangu mchukue mikopo inayotambulika na serikali msichukue mikopo ya kausha damu mikopo hii wanawake inawaumiza riba yake kubwa”amesema Mhe. Masaburi.
Amesema kuwa wanawake ni kiungo wa familia, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika hatua nyengine Mhe. Masabri amebainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imejipanga kufanya maboresha ya masoko Makuu ikiwemo soko la Temeke Sterio, Tandika pamoja Keko ili kuleta tija katika kufanikisha shughuli mbalimbali ikiwemo kuongeza mapato na kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.
Amesema kuwa masoko hayo yatakuwa ya mfano kwa sababu yatakwenda kuleta wateja wengi Sana, kwa hiyo nawaomba viongoozi wa masoko mlisimamie hili”alisema Janeeth.
Pia Mbunge huyu amewakumbusha wafanabiashara wa masoko hayo kuzingatia suala la usafi katika maeneo yao wanayofanyia biashara ili kisudi maeneo yao yawe kivutio kwa watu wanaofika kutembelea masoko hayo kwa kununua bidhaa pamoja na wafanabiashara wenyewe kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Meneja wa Masoko ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Masoko yaliyopo kwenye Wilaya ya Temeke Bw. Godfrey Asukile, amesema kuwa ukarabati wa masoko hayo matatu Temeke Sterio, Tandika na Keko unatarajia kufanyika mwanzoni mwakani na unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 600.
Amesema kuwa masoko hayo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mapaa machajavu ya soko, mitaro, kizimba cha taka na uongezaji wa matundu ya vyoo pamoja na miundombinu ya soko kwa ujumla.
Amesema kuwa soko la Temeke sterio lina wafanyabishara zaidi ya 5, 000, huku akieleza kuwa Manispaa ya Temeke ina jumla ya masoko 28 kati ya masoko 28 masoko 24 ya serikali na masoko manne ya watu binafsi.
Mhe. Masaburi Janeth leo ameendelezo ya ziara ya kikazi ambapo Disemba 6 mwaka huu alianza ziara kwenye kata ya Pugu, Jimbo la Kibamba na Ubungo, Jimbo la Kawe wilaya ya Kinondoni na Jimbo la Temeke wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo ametoa majiko ya gesi na mkaa mbadala kwa mama lishe na baba lishe wanaofanya biashara ya kuuza chakula kwenye masoko hayo ili kisudi waweze kuachana na matumizi ya kupikia kuni na mkaa.