Jaji Mkuu ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akishiriki kuimba wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki leo kabla hajafungua Mkutano wa JMAT ambao umeanza leo tarehe 19 Desemba 2023 jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mhe. Mustapher Mohamed Siyani( wa pili kutoka kushoto), Rais wa JMAT ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. John Kahyoza(wa pili kutoka kulia) , Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu , Kanda ya Dodoma Mhe. Dkt. Juliana Masabo(kushoto) na Mtendaji wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabrriel(kulia)
Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. John Kahyoza akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano wa JMAT leo tarehe 19 Desemba 2023 jijini Dodoma.
Jaji Mkuu ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa JMAT leo tarehe 19 Desemba 2023 jijini Dodoma.
Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT ) ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. John Kahyoza(kushoto) akiteta jambo na Mtendaji wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabrriel(kulia) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa JMAT leo tarehe 19 Desemba 2023 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Matawi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa JMAT leo tarehe 19 Desemba 2023 jijini Dodoma.
………..
Na Tiganya Vincent-Mahakama-Dodoma
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitaka Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania Bara (JMAT) kuwahimiza wanachama wao kuhakikisha wanabaki ndani ya maadili mema na kutoa huduma zilizo bora na kwa wakati.
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Desemba 2023 wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania Bara (JMAT) jijini Dodoma.
“Wajibu wenu kama JMAT kusimamia na kuhimiza uwazi, uwajibikaji…,” alisema Jaji Mkuu… Wanachama wa JMAT mnao wajibu wa kupeana nasaha, kushauriana na kuwaonya wanachama ambao wanakiuka Kanuni za Maadili kusubiri Kamati za Maadili kushughulikia
Mhe. Prof. Juma aliongeza kuwa Wanachama wa JMAT, endapo wataona wadau wanaoendesha mashauri (kwa mfano, Mawakili wa kujitegemea, Mawakili wa Serikali, Madalali, Wasambaza kumbukumbu wanakiuka maadili ya Taasisi zao, ni jukumu lao kufikisha taarifa kwa vyombo vyao vya kimaadili.
WANACHAMA WA JMAT WAHIMIZWA KUJIENDELEZA KIELIMU.
Jaji Mkuu aliwataka wanachama wa JMAT kuendeleza katika masomo yenye maudhui ambayo yatawawezesha kufanyakazi kwa kuzingatia mahitaji ya Karne ya 21.
“Tusikimbilie kusoma Shahada za UZAMILI au UZAMIVU, zenye maudhui ya zamani. Someni yale ambayo yatawajenga kuweza kufanya kazi katika Karne ya 21. Masomo kama Legal-Tech, Project Management, Business Process Management, ADR, negotiation skills,”alisema.
“Mahakama ya Tanzania tayari kuna mfano ya Maafisa wa Mahakama ambao wamesoma na kujiunga katika maeneo mapya ya masomo akiwamemo Mhe. Dkt Ubena John, sasa hivi ni “Associate Professor Information Technology Law”. Mhe. Desdery Kamugisha kujitambulisha kuwa – Mtaalam wa Court Business Process. Pia Mhe. Jaji Dkt Rumisha ni Mtaalum wa Maboresho, Project Management,” aliongeza.
Aidha , Mhe. Prof. Juma aliitaka JMAT kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama, katika kuhakikisha kuwa wanachama wote hawaachwi nyuma na mabadiliko makubwa yanayoendelea duniani yakiwemo mabadiliko makubwa katika matumizi ya kiteknolojia kwa kuhimiza mufunzo endelevu na elimu endelevu.