Na.Sophia Kingimali, Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba amewataka waandaji wa mtaala wa wakufunzi wa elimu ya fedha kuutafsiri kwa kiswahili mtaala huo ili uweze kueleweka kwa watu wote ili lengo lililokusudiwa liweze kutimia.
Wito huo ametolewa leo Desemba 18,2023 Jijini Dar es salaam wakati akizindua Mtaala wa wakufunzi wa elimu ya fedha waliorasimishwa lengo likiwa kuhakikisha elimu ya fedha inamfikia kila mtanzania mwenye elimu na asie na elimu.
Amesema kuwa elimu ya fedha inapaswa kumfikia kila mmoja ili aweze kuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa lakini kuepuka kuingia kwenye sitofahamu ambayo inawakuta wengi hasa wanapokwenda kwenye taasisi za mikopo.
“Niwaangize mtaala huu utafsiriwe kwa lugha ya kiswahili na natoa miezi miwili kukamilisha ilo ili uweze kuwekwa kwenye mitandao ya taasisi mbalimbali ambapo itamsaidia kila mtu kuipata elimu hii ya fedha ambayo ni changamoto kwa nchi”amesema Tutuba
Ameongeza kuwa utekelezaji wa mtaala huo unapaswa kuwa endelevu kwani utasaidia kuongeza uelewa kwa wananchi hasa wanaochukua mikopo kwani utawasaidia kujua namna gani ya kuchambua mkataba ikiwemo riba.
Amesema kuwa utekelezaji huo unapaswa kuwa shirikishi lakini pia uwe na ubunifu wa namna ambavyo ujumbe utaweza kuwafikia watu wengi ikiwemo kuandaa clip fupi za mafunzo.
Aidha Tutuba amesesisitiza kuwa wananchi wakiwezeshwa kuwa na ujuzi sahihi wa matumizi ya fedha utasidia wananchi kuepuka matumizi mabaya ya fedha lakini pia kuepuka kuingia kwe mikopo ya inayowaumiza (kausha damu)
Kwa upande wake mmoja wa washiriki amabae anatokea Shirikisho la Taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha nchini Winnie Terry, amesema uwepo wa mtaala huu utasaidia wateja wao kupata elimu pindi wanapochukua mikopo kwani kuna taasisi nyingine azitoi elimu kuhusu riba na hatimae mkopaji anakua anaingia kwenye mtego unaompelekea kushindwa kulipa deni lake au kulipa kwa hasara kubwa.
“Ni kweli wanavyosema kuhusu kausha damu na hii inatokea kutokana na baadhi ya tasisi azisemi ukweli kuhusu riba zao mtu anajikuta anachukua mkopo kwa kusikia asilimia 30 akijia labda kwa wiki mbili au mwezi kumbe Ile asilimia unailipa kwa mwaka kuna wengine wanashidwa kulipa mikopo hiyo sasa mtaala huu ni mwarubaini maana elimu hii itafika kwa watu wote mpaka wajasiliamali wadogo ambao ndio wateja wetu sana”amesema Terry.