MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera
katikati akitazama kikundi cha utunzaji wa mazingira cha Uwamakizi
wakati ametembelea vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza
vyanzo vya
maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku
akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri
wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru
vyanzo vya maji (SLM) kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Wizara Maji
Obadia Kibona.
Mratibu wa mradi wa kunusuru vyanzo vya maji kupitia matumizi bora ya
ardhi (SLM) Mhandisi Maximilian Sereka ambapo alisema mradi huo ulianza
mwaka 2016 sasa wapo ndani ya mwaka wanne kwenye utekelezaji wa mradi
huo.
MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera
kulia akiangalia miti aina ya mitiki iliyopandwa kwenye Kijiji cha
Sembekeza wilayani Muheza wakati alipotembela vikundi vya uwamakizi na
kuona namna wanavyotunza vyanzo vya
maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku
akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri
wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru
vyanzo vya maji (SLM).
MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera
katikati akionyeshwa namna miti ya mitiki inavyopandwa wakati
alipotembela vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza vyanzo
vya
maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku
akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri
wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru
vyanzo vya maji (SLM).
Mtaalamu wa Mazingiwa Tanga Uwasa Ramadhani Nyambuka kushoto
akisisitiza jambo kwa MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya
Maji George Mvomera
Mhandisi Rashid kutoka Tanga Uwasa kushoto akiwaongoza wataalamu mbalimbali
MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera akitazama namna miche ya mitikiti inavyopandwa
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufika kwenye ofisi za Umoja wa Wakulima Wahifadhi wa Mazingira Kihuhwi Zig
Kikundi cha Uwamakizi kikitoa burudani
Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali
MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera ametembelea vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM).
Mradi huo unasimamiwa na Wizara ya Maji chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambao umeweza kusaidia utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwemo upandaji wa miti kwenye maeneo husika na hivyo kufanya maeneo hayo maji kutiririka mwaka mzima.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo ikiwa ni wiki ya mazingira, Mvomera alioneshwa kuridhishwa na utunzaji wa mazingira unaofanywa na Uwamakizi huku akiwataka wananchi kote nchi kujiunga kwenye vikundi vinavyojihusisha na namna ya kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji ikiwemo kupanda miti rafiki inayotunza maji katika kipindi cha kiangazi.
Alisema wameona kazi kubwa na nzuri inayofanyika kwenye eneo hilo kwani miaka ya nyuma mito hiyo ilikuwa haititirishi maji lakini sasa hivi kutokana na uwepo wa utunzaji wa mazingira maji yameanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida na hilo ndio lengo lao nchi nzima wananchi wajiunge kwenye vikundi na kujihusisha na namna ya kutunza mazingira leo.
“Lakini katika kusheherekea wiki ya mazingira lengo la mwaka huu ni kuhamasisha wananchi kmuacha kutumia mifuko ya plastic lakini pia tumejifunza mengi zaidi miti inayopandwa lazima iweze rafiki kwenye utunzani wa vyanzo vya maji kwani inachangia uwepo wa maji kwenye mito kipindi cha kiangazi”Alisema.
Mkurugenzi huyo alisema miti hiyo inasaidia kufanya mito kutiririsha maji mwaka mzima kwenye maeneo ya vyanzo hizyo huku akikipongeza kikundi cha Uwamakizi kwa kuhifadhi mazingira na Mto Zigi na mito mingine midogo inayoingiza maji kwenye mto huo.
Aidha alisema pia wanategemea kuanzisha mfuko wa maji (Water Fund) kwenye eneo la Uwamakizi kwa kushirikiana na Tanga Uwasa na wadau wengine kuunda mfuko huo ili mradi huo uwe endelevu uhifadhi wa mazingira uendelea kwenye maeneo mengi zaidi ya bonde dogo la mto Zigi ambayo ni sehemu ya bonde la Mto Pangani.
“Niwapongeza uwamakizi kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini nitoe wito maeneo mengine Tanzania waende kujifunza uwamakizi namna ya kutunza vyan zo vya maji namna inavyoileta faida kwa wananchi wanalima kokoa mitiki inayowezesha kujiongeza kipato na kutunza maji kwa kupanda mazao mbadala ya mahindi na maharage ambayo yangewezea kuharibu vyanzo hivyo”Alisema.
Hata hivyo alisema Wizara ya Maji imekuwa ikisaidia maeneo mengi kuanzisha vyama vya watumiaji wa maji kwa nguvu ya wizara maeneo mengine wa usafiri na ofisi faida za jumuiya za watumiaji maji zinasaidia kutatua changamoto za utunzaji wa maji na mazingiea eneo la uwamakizi watafanya kila njia kuwatafutua usafiri wa pikipiki kwa sababu ni eneo kubwa kupitia mradi wa kunusuru.
Naye kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kunusuru vyanzo vya maji kupitia matumizi bora ya ardhi (SLM) Mhandisi Maximilian Sereka alisema mradi huo ulianza mwaka 2016 sasa wapo ndani ya mwaka wanne kwenye utekelezaji wa mradi huo.
Alisema mradi huo unatekelezwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Maendeleo Dunia (UNDP) pamoja na Mfuko wa Mazingira (GF) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji kwa kushirikiana na sekta mbalimbali wamepata mafanikio mengi ikiwemo utoaji wa elimu kwenye maeneo yote mawili Ruvu na Zigi hivyo kuwafanya wananchi kuwa na uelewa mkubwa ukilinganisha na kipindi wanaanza mradi.
Mratibu huyo alisema pia kumekuwepo na ushirikianao kwenye sekta mbalimbali wakati wa utekelezaji wa mradi huo ambao unaratibiwa na sekta ya maji kwa kushirikiana ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara ya Kilimo,Mifugo,
“Lakini pia sekta za serikali mbalimbali ikiwemo mamlaka za maji ya Tanga Uwasa,Moruwasa na Dawasa lakini pia wilaya mbalimbali wanazoshirikiana nazo kwa ukaribu zaidi wilaya za Tanga na Morogoro”Alisema