Wananchi wametakiwa kutumia mvua zinazoendelea kunyeesha kwaajili ya shughuli za kilimo
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula alipotembelewa na mwandishi wetu shambani kwake jijini Dodoma kujionea namna zao la Zabibu linavyoweza kulimwa kisasa kwa kufuata ushauri wa kitaalamu ambapo amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia vizuri mvua zinazonyeesha maeneo mbalimbali nchini kwa kulima na kutunza chakula ili kiweze kuwasaidia
‘.. Mvua zinanyesha maeneo mengi kikubwa tutumie mvua hizi kwa kufanya shughuli za kilimo, Tukifanya vizuri shughuli za kilimo tutapata chakula lakini pia tutauza kupata fedha kwaajili ya mahitaji mengine ..’ Alisema
Aidha Dkt Mabula amewataka wataalam wa Kilimo kuwatembelea wakulima katika maeneo yao na kuwapa elimu itakayowasaidia katika kufanya kilimo bora chenye tija
Wananchi wa Jimbo la Ilemela wanajishughusha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kiuchumi ikiwemo uvuvi, biashara, ufugaji na wengi zaidi wakijihusisha na kilimo