Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) leo imekutana na Menejimenti ya Shirika la Nyumba Zanzibar(ZHC) ili kufahamiana na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuwahudumia watanzania wa pande zote za Muungano katika sekta ya nyumba. Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi ya NHC Dkt Sophia Kongela ameishukuru Bodi na Menejimenti ya ZHC kwa mwaliko wao na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta ustawi wa wananchi wanaohudumiwa na mashirika hayo mawili. NHC imeshiriki mara kwa mara kutoa mafunzo kwa ZHC ya namna ya kuendesha Shirika hilo la nyumba ili kuleta tija.