Mkuu wa Wilaya ya Arusha ,Felician Mtahengerwa akizungumza katika mahafali hayo jijini Arusha.
Mkuu wa chuo hicho,Lazaro Thobias akizungumza na wazazi pamoja na wahitimu katika mahafali hayo.
Wahitimu wa kozi mbalimbali chuoni hapo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Arusha wakati akizungumza katika mahafali hayo.
.,……….,
Julieth Laizer,Arusha .
Arusha .Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Felician Mtahengerwa amevitaka vyuo vya utalii nchini kutoa wahitimu bora wenye viwango vya kimataifa watakaoweza kukidhi na kushindana na soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akiwa katika mahafali ya 5 ya ngazi ya cheti katika chuo cha utalii cha Volcano kilichopo Sakina jijini Arusha ambapo jumla ya wahitimu wapatao 87 wa fani mbalimbali ikiwemo utalii,Mapishi,Ususi,Fundi Umeme na Magari walihitimu na kutunukiwa vyeti.
Mtahengerwa amesema pamoja na kukipongeza chuo hicho kwa namna kinavyotoa elimu na ujuzi, amesema jitihada zaidi zinahitajika kumudu ushindani katika sekta hiyo kwa kutoa wahitimu .
Amesema changamoto hiyo itamalizwa na vyuo iwapo vyuo hivyo vitabadili ifundishaji na kujikita kwenye ubunifu wa kimataifa ikiwemo kufundisha suala la Lugha za kimataifa ili kwendana na soko la ushindani duniani.
Aidha ametoa rai kwa wahitimu kuitumia elimu walioipata , kwenda kufanya ubunifu wenye tija na hadhi ya kimataifa ,namna ya kuanzisha na kuendesha biashara kwa kiwango cha tofauti kwa kujua wanalenga nini ili kukidhi mahitaji ya wateja wao .
“Sasa hivi kuna changamoto kubwa sana ya ajira kwa vijana wetu ,hivyo sisi kama chuo tunatakiwa tuwapatie wanafunzi wetu elimu ambayo itawasaidia kukidhi soko la ajira ndani na nje ya nchi na kuweza kuajirika kwa urahisi zaidi.”amesema .
Naye Mkuu wa chuo hicho ,Lazaro Thobias amesema chuo cha Volcano kimejikita kuzalisha wahitimu wenye viwango vya juu na wengi wa wahitimu zaidi ya asilimia 90 tayari wapo kwenye soko la ajira katika sekta mbalimbali mkoani hapa.
“Sisi chuo cha Volcano tunawaandaa vijana vizuri kwa kuwafundisha ujuzi unaoendana na teknolojia za kimaiaifa na wanaweza kufanya kazi popote duniani kwani tunawafundisha pia lugha mbalimbali za kibiashara za kimataifa”amesema.
Nao baadhi ya wahitimu, Charles Wambura mhitimu waongoza watalii na Rahma Dickson aliyehitimu Mapishi walisema elimu walioipata imewasaidia kuwa na uelewa wa masuala ya utalii na kukishukuru chuo hicho kwa kuwapatia elimu bora na kwa sasa tayari wanaajiriwa.