NJOMBE, Muungano wa vikundi vya wakulima wa Miti Tanzania TTGAU wenye vikundi 154 nchi nzima kwa kushirikiana na shirika la Chakula Duniani FAO umefanya mkutano wa mwaka 2023 mjini Njombe ili kufanya ufatiliaji na Kujifunza utekelezaji wa shughuli za mradi wa miaka 5 Forest Farm Facility(FFF) wenye lengo la Kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi pamoja na Kukuza kipato cha wakulima wa mazao na misitu.
Akizungumzia utofauti wa mradi huo na miradi mingine Timbulo amesema umekuwa na matokeo ya moja kwa moja kwasababu unatekelezwa na wakulima wenyewe licha ya elimu na ujuzi kutolewa kwa wataalamu na wakulima
Timbula amesema kupitia mradi huo wakulima na watalaamu wanajengewa uwezo kulingana na changamoto zinazokwamisha maendeleo yao kwenye suala la chakula,Mazingira ,Mabadiriko ya tabia ya nchi,Kubuni mipango endelevu ili kukabiliana na mabadiriko hayo sambamba na kujengewa uwezo wa kushirikiana na na taasisi binafsi na serikali katika masuala ya maendeleo.
“Mabadiriko ya tabia ya nchi yamesababisha mvua kuchelewa kunyesha,Jua kuwa kali zaidi msimu wa kiangazi na maji kukimbia mabondeni ,sisi tunaangalia leo hatutambui kwanini waliyo tutangulia walilinda vyanzo hivi,hivyo kwa kupitia mradi wa FFF wakulima wanapatiwa elimu na kisha kuanza kuacha tabia ya kulima katika vyanzo na kukata miti hivyo,alisema Timbula “
Awali mwakilishi wa mkurugenzi wa idara ya misitu na nyuki Emma Nzunda ambaye afisa misitu kutoka wizara ya maliasili na utalii akifungua mkutano huo amesema serikali kwa kushirikiana na FAO ilikuja na mradi huo ili kunusuru kasi ya mabadiriko ya tabia ya nchi na kisha kuwataka wakulima kutumia fursa ya mkutano huo kupeana uzoefu,changamoto za utekelezaji wa mradi pamoja na kuweka mikakati ya kufikia maendeleo endelevu.
Nzunda amesema katika kipindi cha miaka mitatu ambayo mradi umetekelezwa tayari mwanga umeanza kuonekana katika mapambano dhidi ya mabadiriko ya tabia ya nchi na kisha kudai kwamba hadi kufika 2025 utamatika ni wazi kwamba vikundi vya wakulima vitakuwa vimeimarika huku pia akiwataka viongozi wa vyama hivyo kuendelea kuhamasisha ufihadhi kwa kupanda miti na ufugaji wa nyuki ili kutengeneza pia kipato cha wakulima.
Mbali na suala la Utunzaji wa mazingira afisa huyo kutoka wizara amejibu hoja ya wakulima wa miti juu ya changamoto ya soko la uhakika na bei elekezi ya mbao ili kudhibiti madalali wanafata wakulima shambani na kisha kununua mbao kwa bei ndogo ili kutengeneza faida ambapo anasema tayari serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa soko kubwa la mbao Iringa na Kiwanda cha mbao Mafinga ili kusogeza soko kwa wazalishaji wa mikoa ya Nyanda za Juu kusini.
“Ni matarajio yangu mwisho wa mradi huu tunakwenda kuona maendeleo makubwa katika mapambano dhidi ya mabadiriko ya tabia ya nchi na uchumi wa wakulima,alisema Emma Nzunda “
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa Forest Farm Facility(FFF) Nchini Godfrey Bakanga ameipongeza TTGAU kwa kuandaa mkutano huo kwasababu kupitia jukwaa hilo vyama vya wakulima kutoka mikoa mbalimbali vilivyo chini ya mwamvuli wa taasisi hiyo vinapata fursa ya kuonesha mafanikio na changamoto vilizokutana nazo wakati wa utekelezaji wa mradi na kisha kupata nafasi ya kujengewa uwezo zaidi.
Nae afisa misitu mkoa wa Njombe Gumbo Mvanda amewataka wakulima na wakazi wa Njombe kuacha kusababisha mioto kwasababu imekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira kwasababu licha ya asilimia 45 ya pato la mkoa huo kutoka kwenye mazao ya misitu lakini katika kipindi cha mwaka 2022/2023 majanga ya moto yamesababisha hasara ya bil 400
“Licha ya kutunga sheria kali za moto lakini bado kuna watu wachoma moto na kusababisha hasara kubwa hivyo tunaamini kupitia mradi huu elimu inayotolewa itapunguza tatizo hilo na kutunza mazingira yetu,alisema Mvanda”
Nao wawakilisha wa wakulima akiwemo Damian Kasulumo Kutoka Mwiwaarusha na Laurent Mfugale ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wakulima wa miti Matembwe ambaye pia mwenyekiti wa bodi wanasema wanaamini kupitia mafunzo ya siku tatu za uzoefu watakao barishana watakwenda kufanya vyema mradi huo huku pia wakihimiza udhibiti wa madalali wa mazao na kuanzisha masoko ya uhakika ya ndani na nje .