Mwanzilishi na Mlezi wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama (BST) mwaka 2023 ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) Profesa Peter Msola akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu wa mwaka 2023 ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es salaam.
Mbunge na Waziri Mstaafu Profesa Jumanne Maghembe akiwa amehudhuria katika mkutano mkuu wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) wa mwaka 2023 ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) ambao wamehudhuria katika katika mkutano mkuu wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) wa mwaka 2023 ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es salaam.
Picha ya Pamoja akiwa Mwanzilishi na Mlezi wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima,pamoja na viongozi mbalimbali baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) wa mwaka 2023 ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es salaam.
……………….
NA MUSSA KHALID
Wadau wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) wametakiwa kujadili fursa na mchango wa kutumia sayansi katika ubunifu ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti ili kufanya malengo yao kuwa na tija.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanzilishi na Mlezi wa Chama hicho ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama hicho mwaka 2023 ambao umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es salaam
Aidha RC Malima amewasisitiza wanasayansi hao kuhakikisha wanakuwa na umoja wa kutengeneza nguvu ya pamoja ya kuipigani fani yao ili kusaidia kupiga hatua katika maendeleo ya nchi.
RC Malima amesema BST inatakiwa ibadilike ili watu waitazame kuwa inashiriki katika huduma mbalimbali za kimaendeleo ili kukuza uchumi wa Tanzania.
‘Wadau wote tunaamini na tunaelewa kwamba maendeleo ya sayansi ndani ya jamii yetu ya Tanzania yatakuwa ni kichocheo kikubwa katika mapinduzi ya kilimo,viwanda pamoja na afya nk”amesema Mwanzilishi wa BST
Amesema kuwa Chama hicho cha kisayansi kinaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania kwani maendeleo ya sayansi yanaendana na utashi mkubwa wa kisiasa.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST) Profesa Peter Msola amesema kuwa waliamua kuanzisha chama hicho ili kusaidia kuchochea mapinduzi ya kilimo na viwanda.
Profesa Msola amesema lengo la chama hicho ni kuendelea kupanua wigo wa kukuza sayansi ili iweze kuhusika katika uzalishaji wa vitu mbalimbali yakiwemo ya uzalishaji wa mimea.
Kwa upande wake Mbunge na Waziri Mstaafu Profesa Jumanne Maghembe amesema Bioteknolojia imekuwa ikitumika katika nyanja mbalimbali ikiwemo madawa yanayotumika kutibu magonjwa.
Katika Mkutano huo wamehudhuria wadau kutoka taasisi mbalimbali mbalimbali za serikali na zisizozakiserikali ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,COSTECH,AATF,Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Chuo Kikuu cha Kilimo SUA na MUHAS.