Na Sophia Kingimali,Dar es salaam.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa mlMamlaka ya Usafiri wa Anga nchini(TCAA),Teophory Mbilinyi,amesema kufuatia juhudi za serikali katika sekta ya anga imepelekea hali ya usafiri wa anga nchini kuimarika jambo ambalo limeifanya anga la Tanzania kuwa salama.
Mbilinyi ameyasema hayo leo desemba 7,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa maazimisho ya siku ya Anga Duniani ambayo uazimishwa kila mwaka ifikapo Desemba 7.
“Anga letu ni salama tunavyovifaa vya kisasa ,kwani tulifunga Rada nne,zote hizi juhudi za serikali katika kuhakikisha kuna usalama kwenye Anga”Amesema Mbilinyi.
Hata hivyo,Mbilinyi,amesema kwa jitihada wanazofanya TCAA imeipelekea nchini kushika namba nne Afrika katika usalama wa Anga.
“Sisi kiteknolojia tupo vizuri,Rada yetu ni Miongoni mwa Rada bora kabisa,na hii imetufanya tuwe namba nne kwa Ubora Afrika”Amesema Mbilinyi.
Kwa Upande wake,Mkurugenzi huduma za Uongozaji wa Ndege,kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini(TCAA),Frola Mwashinga,amesema kwa sasa mamlaka hiyo imewezesha kufungwa kwa mradi mkubwa wa sauti na kubainisha kuwa hapo mwakani hali ya usikivu utaimarika.