MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KATIBU
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi
Cyprian Luhemeja, ameelekeza Menejimenti ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji ili
kuchochea uchumi na fursa za ajira nchini.
Mhandisi
Luhemeja amesema hayo, alipofanya ziara ya kiutendaji katika Ofisi ndogo za
Makao Makuu ya PSSSF, jijini Dar es Salaam, ambapo, pamoja na kujionea shughuli
za utoaji huduma, pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimengti ya Mfuko huo
ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, CPA. Hosea Kashimba.
“Kuna
kundi la vijana, kundi ambalo halina matumaini, zamani wahitimu wa chuo kikuu walikutana
na ajira, lakini sasa hivi hali hiyo ni tofauti kidogo.” Alifafanua.
Alisema, PSSSF ni Mfuko mkubwa, hivyo una jukumu la kuwasaidia wastaafu, lakini pia
kujenga mazingira ya kuwawezesha wastaafu wengi siku za usoni.
“Fungueni
viwanda vingi, vitasaidia kutengeneza ajira kwa vijana, unaposaidia watu wengi na wewe unajisaidia.”
Alifafanua.
Pia
ameelekeza Menejimenti ya PSSSF, kuendelea kutoa elimu kwa umma, ili wananchi
waweze kufahamu kazi kubwa ambayo imefanyika toka kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSPF, PPF, GEPF na LAPF na kuanzishwa PSSSF.
“Kazi
kubwa na nzuri imefanyika kwa kipindi cha miaka mitano toka kuunganishwa kwa
Mifuko, utendaji umeboreshwa kwa kiasi kikubwa, ni muhimu watanzania waweze
kuelewa kazi ambayo Serikali inafanya kwa niaba yao” alisema Mhandisi
Luhemeja.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, amesema, yeye na
Menejimenti yake kwa ujumla wameyapokea maelekezo hayo na ameahidi kuyafanyia kazi.
“Tayari tumewekeza kwenye maeneo ya uzalishaji ya viwanda, tumewekeza kwenye
Machinjio ya kisasa, Nguru, kule Mvomero, Mkoani Morogoro, kiwanda cha Kuchakata Tangawizi, Mamba Miamba
kilichoko Wilayani Same, Mkoani
Kilimanjaro, kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi, Kilimanjaro (KLIC),
kilichoko mjini Moshi na Kiwanda cha Chai Mponde, kilichoko Wilayani Lushoto
Mkoani Tanga, na kama aivyoelekeza Katibu
Mkuu, wetu, tufanye utafiti wa kina, ili kuendelea kuwekeza katika maeneo mengi zaidi na
hivyo tutakuwa tumetimiza azma ya serikali ya kuzalisha ajira nyingi zaidi kwa
watanzania.”Alisema CPA, Kashimba.
Aidha
CPA. Kashimba amebainisha kuwa tokea kuunganishwa kwa Mifuko, uhai wa PSSSF
sasa unaonekana, kwani Mfuko umeweza kulipa madeni yote iliyorithi toka Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii ya awali.
“Ukuaji
wa Mfuko umefikia kiasi cha trillioni 8, lakini pia gharama ya uendeshaji
imepungua kwa asilimia 50 na hivyo tumeokoa kiasi kikubwa cha fedha na kwakweli,
jambo ambalo limeboresha utendaji kiasi kikubwa” alisema, CPA Hosea Kashimba.
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi
Cyprian Luhemeja (kushoto) akizungumza na Menejimenti ya PSSSF, ikiongozwa na
Mkurugenzi wake Mkuu, CPA. Hosea Kashimba (kulia)
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi
Cyprian Luhemeja (katika), akiwa na Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, CPA. Hosea Kashimba
(kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Paul Kijazi.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi
Cyprian Luhemeja, akipoewa maelezo ya kiutendaji ya huduma kwa wateja, kutoka
kwa msimamizi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, PSSSF, Ilala, Bi. Mathilda
Nyallu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi
Cyprian Luhemeja, akipokea mkoba wenye
taarifa mbalimbali za kiutendaji za Mfuko, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF,
CPA Hosea Kashimba.
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi
Cyprian (katikati waliokaa), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Frank Kilimba (wakwanza kushoto waliokaa), Mkurugenzi
Mkuu PSSSF, CPA. Hosea Kashimba 9wakwanza kulia waliokaa), wakiwa katika picha
ya pamoja na Menejiment ya PSSSF.